Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko 20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara
Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the love

MVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara katika mkoa wa Manyara baada ya kuripotiwa vifo 20 vilivyosababishwa na mafuriko katika eneo la Katesh na Gendagi wilayani Hanang mkoani humo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja idadi ya majeruhi kutokana na mafuriko hayo wamefikia 70. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mafuriko hayo yaliyojaa tope yamesababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Jumapili tarehe 3 Desemba 2023 baada ya kuporoka kwa sehemu ya Mlima Hanang.

Mayanja amesema hadi kufikia saa 7.30 mchana wa leo Jumapili, miili 20 imepatikana na majeruhi 70 wanatibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini.

“Uokoaji unaendelea katika maeneo ya Katesh na Gendabi ambapo mafuriko hayo yamepita na kusomba nyumba kadhaa, maeneo ya biashara na kituo kikuu cha kabasi cha Katesh, vifo mpaka sasa vimefika 20,”amesema.

Ameongeza kuwa uokoaji unaendelea kwa kufukua tope ambalo limefunika nyumba, maduka na maeneo mbalimbali.

Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hanang, Rose Kamili amesema zoezi la uokoaji linaendelea ijapokuwa bado ni gumu hasa ikizingatiwa maeneo mengi hayafikiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

error: Content is protected !!