Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Dodoma: Kila kaya, taasisi zilime heka 2 mazao ya chakula
Habari za Siasa

RC Dodoma: Kila kaya, taasisi zilime heka 2 mazao ya chakula

Spread the love

KATIKA harakati za kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuhamasisha  wananchi kulima mazao yenye tija ili kuondokana na baa la njaa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameagiza kila kaya na taasisi ikiwamo shule zilime heka mbili za mtama pamoja na mazao mengine ya chakula katika msimu wa kilimo 2023/2024.

Ametaja mazao hayo yanayopewa kipaumbele kuwa mbali na mtama, ni uwele, mpunga, mhogo, viazi vitamu, maharage, kunde, mbaazi, njegere, choroko, viazi mviringo na mahindi. Anaripoti Danson Kaijage, Mpwapwa (endelea).

Senyamule ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Novemba 2023 katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa kilimo 2023 /2024.

Uzinduzi huo umehusisha wataalamu, maafisa kilimo kwa lengo la  kusaidia wakulima kulima kilimo cha uhakika wa chakula, afya bora, ajira na kukuza uchumi kwa mtu mmmoja mmoja na Serikali.

Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 29 Novemba 2023 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mazae Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Amesema malengo ya msimu wa kilimo 2023/2024 ni kila kaya na taasisi kama shule lazima kulima angalau heka mbili za mtama.

Ameongeza kuwa matarajio ni kulima tani 170,235 za mazao ya biashara ni alizeti, korosho, karanga na ufuta tani 13,350.

Aidha, Senyamule ametoa wito kwa maafisa Kilimo kufanya hamasa ya kutosha kijiji kwa kijiji kwa kulima kufanya shughuli za kilimo, kufanya kazi ya kuwapimia udongo wananchi ili kuwasaidia kujua aina ya mazao ya kulima kwenye mazingira yao pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa mbegu bora na kuwaunganisha na taasisi za kilimo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu ametoa wito kwa wakulima wote wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla kuzingatia elimu wanayopewa na wataalamu wa kilimo ili kuongeza uzalishaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!