Wednesday , 22 May 2024
Home Habari Mchanganyiko KKKT: Viongozi msitumie madaraka kutesa watu
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

KKKT: Viongozi msitumie madaraka kutesa watu

Askofu Jacob Mameo
Spread the love

Askofu Kanisa la Kiinjili, Kilutheri Tanzani (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Jacob Mameo ametoa wito kwa viongozi wenye tabia ya kutumia vibaya madaraka  yao kuwakandamiza na kuwatesa watu wa tabaka la chini, kuacha tabia hiyo kwani sio tu chukizo kwa binadamu bali pia ni chukizo kwa Mungu Anaripoti Victor Makinda, Morogoro …(endelea).

Askofu Mameo ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la uzinduzi wa siku 16 za kupinga katili wa kijnisia lililoandaliwa na kanisa hilo.

 Amesema wapo baadhi ya viongozi katika jamii ambao huyatumia vibaya madaraka yao kwa kuwakandamiza, kuwanyanyasa na kuwaumiza wengine kimwili na kihisia kinyume  sheria na taratibu za nchi na pia kiunyume na mafundisho ya dini zote.

“Vitabu vitakatifu vinaeleza kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo ni lazima maisha yetu yaenzi kusudi la uumbaji wa Mungu la kuishi kwa upendo, furaha kuwa sababu ya wengine kufurahia maisha,” amesema Mameo.

Aidha, ameongeza kuwa watawala wote nchini wanatakiwa wamuombe Mungu ili wasiwe chanzo cha kunyanyasa na kuumiza wengine kwa kuwa wana madaraka.

Mwanasheria wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Elisifa Lepilali, akizungumza kwenye kongamano hilo.

Amesema jamii ya Kitanzania na kote duniani iungane na kusema hapana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwani vitendo hivyo huacha makovu makubwa yasiyofutika kwa wahanga.

Kongamano hilo lililowaleta pamoja viongozi wa dini, wanasheria, maafisa ustawi wa jamii wa Manispaa ya Morogoro na waandishi wa habari.

Aidha, Mratibu wa Mipango wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Yona Kitua amesema jamii inatakiwa iendelee kuelimishwa  kwa lengo la kubainisha vitendo vipi vinaangukia katika ukatili wa kijinsia, madhara na nini kifanyike kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia visiendelee kutokea.

“Ili jamii iwe salama pasipo vitendo vya ukatili wa kijinisia, lazima tuendelee kutoa elimu kwa mbinu mbali mbali na bila kuchoka, kwani elimu ndio njia pekee inayoweza kubadili tabia na mienendo isiyofaa  kwenye jamii,” amesema Yona.

Afisa Utawi wa Manispaa ya Morogoro, Fidna Mathias amesema hakuna sababu ya jamii kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwataka watu  wote wanaofanyiwa vitendo hivyo au wanaoshudia mtu anafanyiwa  vitendo hivyo kuripoti kwenye mamlaka husika.

Naye mmoja wa waandishi waliohudhuria kongamano hilo, Omary Hussen amesema dhima kubwa ya vyombo vya habari ni kusambaza elimu kwa jamii, hivyo wandishi wa habari wanapaswa kuhakikisha ujumbe unaotolewa kuhusu kupinga vitendo vya  ukatali wa kijinsia unaifikia jamii yote.

Aliwaasa waandishi wa habari kote nchini, kuzitumia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kuandaa, makala na vipindi mbali mbali vya kuelimisha jamii kuendeleza mampambano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

error: Content is protected !!