Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amtumbua Naibu Waziri – Pauline Gekul
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia amtumbua Naibu Waziri – Pauline Gekul

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Zuhura Yunus haikueleza zaidi sababu za kutenguliwa kwa Mbunge huyo wa Babati Mjini kupitia CCM.

Kabla ya kutenguliwa kwake, kuanzia jana kumeibuka taarifa katika mitandao ya kijamii zikidai mbunge huyo kuwa anatuhumiwa kumtendea ukatili mfanyakazi wake kijana aliyekuwa anamtuhumu kutaka kumuwekea sumu huko Babati mkoani Manyara.

Ikumbukwe kuwa Gekul ambaye awali alikuwa kada wa Chadema, alipata ubunge mwaka 2015 kupitia chama hicho kabla ya mwaka 2021 kuhamia CCM kisha kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo kabla wizara hiyo haijagawanywa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

error: Content is protected !!