Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule za St Mary’s zang’ara matokeo darasa la saba
Elimu

Shule za St Mary’s zang’ara matokeo darasa la saba

Spread the love

SHULE za St Mary’s nchini zimeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa la saba kwa wanafunzi wake kupata wastani wa alama A kwenye matokeo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wanafunzi wote wa shule hizo wamefaulu kwa alama A na wachache wamefaulu kwa wastani wa alama B.

Mkuu wa Shule ya Msingi, St. Mary’s Tabata Thomas Samson, alisema kuwa siri ya mafanikio ya shule hizo ni kuwa na walimu bora wanaotambua wajibu wao na kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wanaelewa.

Wanafunzi wa shule ya msingi St Mary’s Mbezi wakifurahia baada ya Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Alfred Kata kuwatangazia matokeo ya shule hiyo ya darasa la saba ambapo wanafunzi wote walifaulu kwa alama A na wachache alama B leo shuleni hapo.

Alisema walimu wa shule hiyo wamefanyakazi kubwa ya kuwaandaa wanafunzi wake kwa kuwapa mitihani ya majaribio ya mara kwa mara hivyo wanafunzi wake kufaulu mitihani ya darsa la saba haijawashangaza.

Alisema walianza kuona dalili nzuri ya kufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo baada ya kuwa wanafanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya majaribio ya kimkoa na  kiwilaya ambapo nako walikuwa wanapata wastani wa alama A.

“Sisi tunachojua ni kufundisha, mzazi ukitukabidhi mtoto wako ukae ukijua kwamba umemleta sehemu sahihi kwasababu hata kama angekuwa ni slow leaner tutamfundisha mpaka atakwenda na kasi ya wenzake wenye matokeo mazuri,” alisema

Wanafunzi wa shule ya Msingi St Mary’s Tabata wakifurahi baada ya Naibu mkuu wa shule hiyo, Laizer Yassin (mbele) kuwatangaziwa matokeo ya shule yao ya darasa la saba ambapo wanafunzi wake wote wamefanikiwa kufaulu kwa alama A kwenye matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA).

Naye Mkuu wa Shule ya Msingi St Mary’s Mbezi, Isaac Tamaro,  alisema amefurahi kuona wanafunzi wake wamefaulu kwa kiwango cha juu na kuahidi kuwa hawatabweteka na matokeo hayo na badala yake wataongeza juhudi.

“Siri ya ufaulu huu ni moja tu kufundisha na kuwawekea wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunza kwa kuwapa vitabu vya kutosha na walimu wenye kujua wajibu wao kwamba ni kufundisha tu na kwa kweli matokeo ya juhudi zetu tumeyaona nawapongeza walimu,” alisema

Wanafunzi wa shule ya St Mary’s wakifurahia matokeo ya darasa la saba ya shule hiyo ambapo wanafunzi wa shule hiyo walifanikiwa kupata alama A na wachache alama B kwenye matokeo ta darasa la saba yaliyotangazwa na NECTA jana.

Isaac alisema wanafunzi  wa shule za St Mary’s wamekuwa wakipewa motisha mbalimbali wanapofanya vizuri ikiwemo kupelekwa kwenye mbuga za wanyama kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na Ruaha kwaajili ya kutalii na kujionea wanyama mbalimbali.

“Tunaushukuru uongozi wa shule za St Mary’s kwa kuendelea kujali walimu wake na kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusomea binafsi naona hii imekuwa chachu ya mafanikio haya na tunawashukuru wazazi kwa kutuamini na sisi tunawaahidi kwamba tutaendelea kufanya vizuri zaidi,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

error: Content is protected !!