Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wasichana, wavulana wakabana koo ufaulu darasa la 7
ElimuTangulizi

Wasichana, wavulana wakabana koo ufaulu darasa la 7

Spread the love

TOFAUTI na miaka iliyopita, katika matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2023 (darasa la saba) yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), yameonesha ufaulu wa wavulana na wasichana umefanana ambapo wavulana wamefaulu kwa asilimia 80.59 na wasichana wamefaulu kwa asilimia 80.58. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Matokeo hayo yaliyotangazwa leo Alhamisi na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohamed, jumla ya watahiniwa 1,092,960 sawa na asilimia 80.58 ya watahiniwa 1,356,296 wenye matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2023 wamefaulu ambapo wamepata madaraja ya A, B, na C.

Wavulana waliofaulu ni 507,920 sawa na asilimia 80.59 na wasichana waliofaulu ni 585,040 sawa na asilimia 80.58.

Mwaka 2022 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 1,073,402 sawa na asilimia 79.62. Hivyo, ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.96.

Katika ubora wa ufaulu, watahiniwa wengi wamepata daraja la B na C ambapo daraja la B ni watahiniwa 314,646 (23.20%), daraja la C ni watahiniwa 724,371 (53.41%). Aidha, watahiniwa 53,943 (3.98%) wamepata daraja la A.

Ubora wa ufaulu kwa wasichana umeongezeka kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 80.58 ikilinganishwa na asilimia 78.91 katika mwaka 2022 ambapo ongezeko katika daraja la A ni asilimia 0.13, daraja la B ni asilimia 0.96 na daraja la C ni asilimia 0.57.

Ubora wa ufaulu kwa wavulana umeongezeka hadi asilimia 80.59 ikilinganishwa na asilimia 80.41 katika mwaka 2022 ambapo ongezeko katika daraja la A ni asilimia 0.42 na daraja la B ni asilimia 0.58. Aidha, ufaulu wa daraja la C umeshuka kwa asilimia 0.83.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Hatuoni faida ya demokrasia

Spread the loveMwenyekiti wa Chadema, Fremaan Mbowe amesema Tanzania haijanufaika na miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ataka wananchi wasiruhusu bakora za Magufuli

Spread the loveMwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahimu Lipumba...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mbunge Mwakasaka alitaka Jeshi la Polisi kutenda haki

Spread the loveEMMANUEL Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), amelitaka Jeshi...

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

error: Content is protected !!