Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu CBE, DSE kuwapa wanafunzi mbinu za masoko
Elimu

CBE, DSE kuwapa wanafunzi mbinu za masoko

Spread the love

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeingia makubaliano na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ya kuwapa mafunzo ya vitendo wanafunzi wake kwa kuwapa mbinu za masoko ya mitaji na ya ajira ili waweze kujiajiri na kuajirika baada ya kujitimu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wanafunzi watapewa mafunzo hayo kupitia shindano la uwekezaji kwa njia ya hisa chini ya (DSE Scholar Investment Challenge), ambapo watasimamiwa na (mentors) kwa kununua na kuuza hisa kwa fedha mtandao (virtual money).

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tandi Lwoga, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya marekebisho makubwa yaliyofanywa kwenye mitaala ya chuo na kufanya somo la uwekezaji na fedha kuwa la lazima.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga (kulia) na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE Mary Mniwasa wakigonga kengele kuashirikia kuanza kwa ushirikiano wa taasisi hizo mbili

“Mwaka jana tulifanya upembuzi yakinifu na kuongeza elimu ya fedha na uwekezaji katika mtaala tunaofundisha na somo hilo la lazima limeanza kufunishwa mwaka huu kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada hivyo uwepo wa shindano hili litawafanya wanafunzi wajifunze kwa vitendo badala ya nadharia darasani,” alisema Profesa Lwoga.

Alisema hilo lilifanyika ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayozidi kutokea kila wakati duniani.

“Mkashiriki, mkajifunze na kuwekeza hizo fedha mtakazopewa ili tuzalishe wawekezaji, waajiriwa na wajasiriamali wenye ujuzi,” alisema Profesa Lwoga.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Mary Mniwasa alisema wamejipanga ili kuhakikisha shindano hilo mwakani linahusisha vyuo vyote nchini ili kuweza kukuza elimu hiyo.

Alisema shindano hilo linalenga kuwaandaa wnafunzi kujua vihatarishi na faida za kuwekeza katika soko la hisa.

“Kitu cha tofauti mwaka huu mtakuwa na madarasa kwa ajili ya uwekezaji na kupitia wasimamizi wenu (mentors) mtaweza kujifunza vitu vingi, pia mtakuwa na klabu mbalimbali katika vyuo vyenu kujadiliana nini mnaweza fanya na ni ruhusa kuwa na klabu zaidi ya moja,” alisema Mniwasa.

Viongozi wa CBE na DSE wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya tukio hilo.

Shindano hilo ambalo litafikia tamati Juni mwakani, litahusisha wanafunzi wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na CBE.

Wanafunzi hao watapewa shilingi milioni moja kwa njia ya mtandao (virtual money) ambayo watapaswa kuizalisha kupitia ununuzi wa hisa na watakaozalisha zaidi watakwenda hatua mbalimbali ikiwemo ya maswali na majibu kuhusu DSE kabla ya mshindi kutangazwa.

Meneja wa Miradi Maalumu kutoka DSE,  Emmanuel Nyalali, alisema lengo la kuandaa mashindano hayo ni kuwafanya wanafunzi kuangalia soko la hisa kama sehemu inayoweza kuwaongezea tija na kuwaandaa kuwa wawekezaji na waajiriwa wenye ujuzi stahiki.

“Ukitafuta kazi  na tayari una ujuzi kuhusu uwekezaji hata anayetaka kukuajiri unamfanya akutazame kama mtu asiyehitaji kutumia nguvu zaidi katika kukuelekeza,” alisema Nyalali.

Alisema tofauti na miaka mingine mwaka huu wanafunzi watakuwa na vikundi kwa ajili ya kubadilishana ujuzi pia watapata usaidizi kupitia wasimamizi (mentors) ambao watakuwa wakiwasaidia juu ya nini wafanye kwa wakati gani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

error: Content is protected !!