Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bweni la Wasichana Hasnuu Makame Sekondari Z’bar lateketea kwa moto
Habari MchanganyikoTangulizi

Bweni la Wasichana Hasnuu Makame Sekondari Z’bar lateketea kwa moto

Spread the love

 

JENGO la Dakhalia la Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame ilioko Kibuteni Wilaya ya Kusini Unguja, limeungua moto sehemu ya juu, imeripotiwa. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, sehemu ya juu ya jengo ambako wanafunzi wasichana ndiko wanalala, imeteketea yote.

MwanaHalisi Digital TV imeelezwa na vyanzo tofauti kuwa dalili za kuzuka moto zilionekana mapema laasir kulipotokea shoti kwenye moja ya vyumba vya kulala wasichana.

Tulifanikiwa kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Unguja, Rajab Mkasaba akieleza kuwa hakuna mwanafunzi aliyedhurika kwa sababu wakati moto unaanza walikuwa eneo la chakula (Dinning Hall) na baadaye waliingia madarasani.

Wanafunzi wawili walikuwa vyumbani kwa dharura ya kuumwa lakini “waliwahi kutolewa kabla ya kuathirika kwa namna yoyote ile.”

DC Mkasaba anasema ghorofa ya juu ya jengo la ghorofa moja ndilo limeungua – limeteketea kabisa.

Jitihada kubwa imefanywa kuokoa moto usilete madhara makubwa lakini hakuna kilichobakia, licha ya askari wa KZU kufanya kazi kubwa, anasema.

Amesema mbali na magari mawili yaliyotoka Kituo cha Zimamoto cha Kitogani, Wilaya ya Kusini, walipata msaada zaidi wa gari kutoka Kituo cha Marumbi na Mjini. Katika mazungumzo yake na MwanaHalisi Digital TV, DC Mkasaba amesema moto ulitokana na hitilafu ya umeme.

Taarifa za walioshuhudia zinasema chanzo ni shoti ya umeme kwenye feni ktk moja ya vyumba vya Dakhalia ya Wanafunzi Wasichana.

Mwananchi aliyezungumza kutoka Makunduchi, ambaye alifika eneo la tukio robo saa tangu moto ulipozuka, anasema hitilafu iliripotiwa saa 10 laasiri lakini akadai hakuna hatua iliyochukuliwa kurekebisha.

“Binti yangu anayesoma Skuli ya Hasnuu Makame amenambia mwenzao alipiga kelele Saa 10 aliposikia sauti kubwa ya shoti kutoka kwenye feni. Alimkimbilia Matron wao na kumpa taarifa lakini taarifa ilipuuzwa.

“Ilipofika Saa moja nikajulishwa kuwa shoti imesababisha moto mkubwa na dakhalia inateketea,” alisema huku akisikitika kwamba kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU) kimekosa ubunifu na vifaa wakati wa jitihada za kuzima moto.

“Nimejionea mwenyewe hawa Zimamoto wamekuja na chupa moja ya dawa. Haikufanya lolote kuuzima moto. Ni aibu hawa wanakuja bila ya sawa ya kutosha,” alisema.

DC Mkasaba alisema maofisa wa kitengo cha maafa kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Elimu walikuwa njiani kufika Kibuteni kwa ajili ya kuchukua hatua zifaazo.

Nilipomuuliza kama watawaruhusu wanafunzi wanaoishi Dakhalia kwenda majumbani kwao, DC Mkasaba alisema hilo ni suala linalohitaji mashauriano na kwamba kikao kwa ajili hiyo kitafanyika haraka iwezekanavyo.

Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame, iliopo hatua chache kutoka njia panda ya kwenda Kizimkazi na Makunduchi kutokea mjini Zanzibar, ina miaka miwili hivi tangu kuanza kutumika.

Nayo ni miongoni mwa skuli za sekondari zilizojengwa wakati wa utawala wa Dk. Ali Mohamed Shein na zote zilipewa majina ya viongozi wa kisiasa wakiwemo marais wastaafu Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!