Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uhaba wa dola, Serikali yaanza kubana matumizi
Habari za SiasaTangulizi

Uhaba wa dola, Serikali yaanza kubana matumizi

Dk. Mwigulu
Spread the love

WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imechukua hatua ya kubana matumizi ya ndani hasa katika maeneo ya matumizi ya kawaida ili kukabiliana na uhada wa dola ya Marekani nchini ambao unaweza kuathiri miradi ya maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Mwigulu amesema hatua hiyo inatokana na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amemtaka kuhakikisha anabana matumizi yasiyo ya lazima ili bajeti ya miradi ya maendeleo iliyopitishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 isiathirike.

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Septemba 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesa (CCM) aliyehoji mpango wa Serikali katika kunusuru uchumi wa nchi kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni hususani dola za Marekani.

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alihoji mpango wa serikali kunusuru bajeti hiyo hasa ikizingatiwa wakati inapitishwa na Bunge, Dola moja ya Marekani ilikuwa Sh 2,350 lakini sasa imepanda hadi 2,600.

Akijibu maswali hayo, Dk. Mwigulu amesema Serikali imeongeza kiwango cha kuuza fedha za kigeni katika soko la fedha za kigeni, ambapo kati ya Machi 2022 na Agosti 2023, Benki Kuu ya Tanzania imeuza katika soko la fedha za kigeni zaidi ya dola zaidi za Marekani milioni 500.

Pia imeongeza vyanzo vya upatikanaji wa fedha za kigeni ikiwemo ununuzi wa dhahabu; kutekeleza mikakati ya kuongeza mauzo nchi za nje na kuzalisha bidhaa mbadala wa zile zinazoagizwa kutoka nje ya nchi na kuendelea kushirikisha benki za biashara, maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, pamoja na wadau wengine katika kusimamia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya usimamizi wa fedha za kigeni hapa nchini.

“Pamoja na changamoto zilizojitokeza hali ya upatikanaji wa fedha za kigeni nchini imeendelea kuwa himilivu ambapo akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani milioni 5,246.7 mwezi Julai 2023, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4.7 ikilinganishwa na malengo ya miezi minne,” amesema.

Majibu hayo ya Dk. Mwigulu yamekuja siku chache baada ya Serikali kuwasilisha ombi Benki ya Dunia (WB) kuharakisha upatikanaji wa zaidi ya Dola za Marekani 500 milioni ifikapo Novemba 2023 ili fedha hizo zisaidie kukabiliana na changamoto ya uhaba wa dola katika mzunguko wa fedha hali inayochangia mfumuko wa bei na kukwamisha uagizaji wa bidhaa ikiwemo mafuta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!