Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wastaafu 1,744 EAC walipwa bilioni moja
Habari za Siasa

Wastaafu 1,744 EAC walipwa bilioni moja

Exaud Kigahe
Spread the love

SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia Septemba, 2023 imelipa jumla ya Sh bilioni moja wastaafu 1,744 wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya serikali kuendelea kulipa pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu ambao hawakuwa kwenye mpango wa kuchangia ambao walirejeshwa na kusajiliwa katika daftari la malipo ya pensheni ya kila mwezi.

Hayo yamesemwa leo tarehe 8 Septemba 2023 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe kwa niaba ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum CCM, Subira Mwaifunga.

Mbunge huyo alihoji, Serikali ina mpango gani wa kuwalipa Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri ameeleza kuwa malipo ya wastaafu hao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliidhinishwa kulipwa kupitia waraka wa Baraza la Mawaziri namba 39 wa mwaka 2006.

Amesema Serikalo iliamua kuwalipa wastaafu hao kwa kuzingatia sheria ya pe na wastaafu walilipwa kwa kuzingatia Sheria za pensheni, za Jumuiya hiyo, Sheria na taratibu za fedha, maridhiano ya mwaka 1984 na Sheria namba 2 ya mwaka 1987, pamoja na Hati ya Makubaliano ya Septemba 2005 na Hukumu ya Mahakama Kuu ya 21 Septemba 2005.

“Kwa kuzingatia miongozo tajwa hapo juu Serikali iliandaa utaratibu na kulipa wastaafu na mirathi kwa waliofariki wapatao 31,831 kwa mujibu wa hati ya makubaliano, zoezi hilo lilifanyika kwa kipindi cha miaka minane kuanzia Julai, 2006 hadi Novemba, 2013 lilipofungwa rasmi,” amesema.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kulipa pensheni kwa wastaafu wanaostahili kulingana na sheria, kanuni na taratibu za malipo ya Serikali na si vinginevyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!