TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeandika historia baada ya kufuza kwa mara ya tatu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 13 Januari hadi tarehe 11 Februari mwaka 2024 nchini Ivory Coast. Anaripoti Mwandishi Wetu ..(endelea).
Taifa Stars imefanikiwa kuandika historia hiyo baada kuwalazimisha wenyeji Algeria suluhu ya 0-0 kwenye Uwanja wa 19 Mei 1956 mjini Annaba leo Alhamisi usiku.
Taifa Stars ilihitaji sare yoyote ili kujihakikishia tiketi ya kucheza fainali hizo dhidi ya Mbweha hao wa Jangwani (Algeria) ambao wameizidi kwa mbali Tanzania katika ubora wa soka barani Afrika.
Mara ya kwanza Tanzania ilishiriki fainali hizo mwaka 1980, mara ya pili mwaka 2019 na sasa inakwenda kushiriki mwaka 2024.
Mbweha hao wa Jangwani (ambao walikuwa wamejihakikishia kufuzu kama washindi wa Kundi F) kwa kushinda michezo yote mitano na kujikisanyoa pointi 15 kabla ya leo kukwaa kisiki kwa Taifa Stars tena wakiwa nyumbani.
Matokeo mengine ya Kundi F, bao 2-0 kutoka Uwanja wa Marrakesh nchini Morocco, yaliifanya Uganda kuishinda Niger, ingawa ushindi wao uliambulia patupu kutokana na juhudi za Tanzania.
Algeria walianza kwa kasi na kutengeneza nafasi za mapema kupitia kwa Fares Chaibi na Aymen Mahious, ingawa hakuna aliyeweza kumsumbua kipa wa Tanzania, Benno Kakolanya.
Taifa Stars ilifanya kazi ya kwanza kulenga lango Mbweha hao katikati ya kipindi cha kwanza baada ya Kibu Denis kumlazimisha kipa wa Algeria, Anthony Mandrea kuokoa shuti lake kali la kushtukiza.

Taifa Star walitoa mashambulizi ya hapa na kabla ya kwenda mapumziko, lakini Mbweha wa Jangwani walifurahia umilki mkubwa wa mpira na kudhibiti mchezo kwa jumla.
VIKOSI HIVI HAPA
ALGERIA: Mandrea, Mandi, Ait Nouri, Tougai, Chaibi, Bouanani (Mahrez 68′), Mahious (Amoura 69′), Van Den Kerkhof, Kadri (Boudaoui 71′), Abdelli (Benrahma 68′), Zorgane (Zerouki 71′ )
TANZANIA: Kakolanya, Mnoga, Hamad, Dickson, Mwamnyeto, Kibu, Msuva (Bocco 90+3’), Bajana, Yassin, Mzize (Suleiman 54’ [Mkami 75’]),
Leave a comment