Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Upinzani Zimbabwe walia rafu uchaguzi mkuu
Kimataifa

Upinzani Zimbabwe walia rafu uchaguzi mkuu

Spread the love

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, ameituhumu serikali ya nchi hiyo kwa udanganyifu na wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumatano. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Chamisa amewaambia waandishi habari mjini Harare, kuwa zoezi la kupiga kura lilighubikwa na vitendo vya udanganyifu na unyanyasaji kwa wapigakura, akigusia hitilafu kadhaa zilizojitokeza ikiwemo kuchelewa kufunguliwa kwa vituo vya uchaguzi.

Amesema chini ya robo ya vituo vyote vya kupigia kura kwenye mji mkuu Harare ndiyo vilifunguliwa kwa wakati.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi iliyosema hali hiyo ilitokana na kuchelewa kwa uchapishaji karatasi za kupigia kura.

Upinzani umeilaumu serikali inayoongozwa na chama cha ZANU-PF, kinachoitawala nchi hiyo tangu uhuru mwaka 1980.

Kwenye uchaguzi huo ambao sasa matokeo yake yanasubiriwa, Rais Emmerson Mnangagwa wa ZANU-PF anayewania muhula mwingine madarakani dhidi ya Chamisa wa chama cha Citizens Coalition for Change (CCC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!