Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Genge la matapeli latua Chamwino, wananchi watahadharishwa
Habari Mchanganyiko

Genge la matapeli latua Chamwino, wananchi watahadharishwa

Spread the love

MTENDAJI wa Kijiji cha Huzi Kata ya Huzi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Sospeter Ngalongwa amewataadharisha baadhi ya watu wanaoingia kijijini hapo kununua ardhi bila kupitia ofisi za viongozi kuwa wataangukia mikononi mwa kikundi cha  matapeli na kupata hasara itakayosababisha migogoro isiyokuwa na sababu. Anaandika Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Kiongozi huyo ametoa rai hiyo leo tarehe 15 Agosti 2023 baada ya kutokea wimbi la madalali katika kijiji hicho ambao wanajifanya wana maeneo wanayoyamiliki na kutaka kuyauza wakati maeneo hayo siyo ya kwao.

Amesema jambo hilolinaweza kusababisha mgogoro na machafuko.

Mmoja wa wasimamizi ya mashamba ambayo yamevamiwa na matapeli, Ndama Maduka akionesha shamba hilo analolimiki.

Akizungumzia malalamiko ambayo yanatolewa na baadhi ya wananchi kwa kuwepo kwa kundi hicho, Mtendaji huyo amesema kuna kikundi cha watu wanne ambao wanapita kwenye maeneo ya watu na kujiwekea mipaka na kujifanya kuwa ni maeneo yao jambo ambalo ni uongo.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Huzi  ambao wamekumbana na adha ya matepeli waliotaka kuuza eneo lake ni mzee Mkhani Makuda ambaye amesema alishangazwa na baadhi ya watu ambao walianza kujigawia ardhi kwa madai kuwa wao ni wamiliki halali jambo ambalo ni udanganyifu.

“Walikuja vijana hapa wakiwa na wateja wakaanza kujigawia maeneo ambayo mimi (Maduka) nayamiliki wakidai kuwa wao ni wamiliki ya maeneo hayo, wakati nilianza kumiliki maeneo hayo zaidi ya miaka nane iliyopita nikiwa naendesha shughuli za kilimo na ufugaji kwa muda huo na nina nyaraka zote za umiliki.

“Baada ya kutokea hali hiyo nilitoa taarifa kwenye ofisi za kijiji na baada ya vijana hao kujua nimeshatoa taarifa kwa uongozi na kuonesha nyaraka za umiliki, walianza kutafuta njia nyingine ya kuuziana kienyeji jambo ambalo mpaka sasa hawajafanikiwa kufanya biashara kutokana kutokuwa na nyaraka yoyote ya mauziano,” ameeleza Mzee Maduka.

Kwa upande wake Ndama Maduka amesema kuwa madalali hao wasipothibitiwa ni wazi kuwa wanaweza kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Hata hivyo, Maduu amesema viongozi wanatakiwa kuingilia kati tatizo hilo kwa haraka kabla ya hali haijawa mbaya.

Kwa upande wake Edward Mdowe ambaye anatuhumiwa na baadhi ya wananchi kwa maelezo kuwa anaongoza kikundi hicho cha matapeli alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikana kuhusika na badala yake alikata aulizwe kamishna wa ardhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Elimu ya utunzaji wa mazingira ipewe kipaumbele kwa watoto

Spread the love  JAMII imetakiwa kuwajengea Watoto tabia ya utunzaji wa mazingira...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

error: Content is protected !!