Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mlinzi aliyehukumiwa kumuua mke wa rais kuachiwa huru
Kimataifa

Mlinzi aliyehukumiwa kumuua mke wa rais kuachiwa huru

Spread the love

MLINZI aliyemuua Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Marike De Klerk, Luyanda Mboniswa anatarajiwa kuachiliwa huru mwishoni mwa mwezi huu. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo, kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Marie alikuwa mke wa Rais Frederik Willem de Klerk aliyeliongoza taifa hilo kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1994.

Mei 2003, mlinzi huyo mwanaume aliyekuwa na umri wa miaka 22, alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kuua na wizi katika nyumba ya Rais huyo.

Hata hivyo, Mboniswa alikutwa na simu, saa ya dhahabu na pesa kisha akakamatwa siku mbili baada ya uhalifu huo na kuhukumiwa kifungo chake cha maisha.

Tukio hilo lilitokea Desemba 2001 ambapo mwili wa Marike De Klerk ulipatikana bafuni katika moja ya jumba lake huku ikiwa na mjeraha ya kuchomwa kisu na kunyongwa nyumbani kwake Cape Town nchini humo.

Hivyo, Idara ya Magereza nchini humo ilitoa masharti na utaratibu wa kuorodhesha makosa ya muda kwa kuyapa msamaha maalum.

“Amezingatiwa kwa kuwekwa kwenye orodha ya msamaha baada ya kutumika muda wa chini unaohitajika na atakubaliwa katika mfumo wa urekebishaji wa kijamii, ambapo anatarajiwa kuachiwa kwa utaratibu maalum wa masharti ya msamaha,” amesema Singabakho Nxumalo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!