Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wataka kibano kwa wanaoajiri watoto
Habari Mchanganyiko

Wataka kibano kwa wanaoajiri watoto

Spread the love

MTANDAO wa kupinga utumikishwaji watoto Tanzania, umeiomba Serikali iweke mikakati itakayosaidia kutokomeza ajira za watoto ili kulinda ustawi wao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito wa mtandao huo umetolewa leo tarehe 12 Juni 2023, jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga utumikwaji watoto.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya mtandao huo, Samatta Ibrahim, amesema licha ya Serikali kuweka sheria zinazolinda haki za watoto, bado changamoto ya utumikishwaji ipo, hivyo inatakiwa kuanza kuwabaini wanaotekeleza vitendo hivyo kwa ajili ya kuwachukulia hatua.

Samatta amesema sekta zinazoongoza kwa kuwatumikisha watoto ni  madini, kilimo, uvuvi na shughuli za majumbani.

Katika hatua nyingine, Samatta amesema changamoto hiyo inatokana na sababu mbalimbali, hususan ya hali duni ya maisha  kitendo kinachopelekea familia kuwaagiza watoto wakafanye kazi kwa ajili ya kujipatia ridhiki.

Amesema ili changamoto hiyo itafutiwe ufumbuzi, Serikali inapaswa kuongeza juhudi za kuwakomboa wananchi kiuchumi hasa wa vijijini ili waweze kutunza familia zao.

Mjumbe wa mtandao huo, Eddna Chandeu,  amesema kwa mujibu wa takwimu za 2020, Tanzania Ina watoto milioni 4.2 wanaotumikishwa hasa kutoka maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Joyce Maketa,  amesema Idara ya ustawi wa Jamii imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuwasaidia watoto wanaobainika kutumikishwa ikiwemo kuwarejesha katika familia zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!