Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya dunia yamwaga Sh. 800 bilioni kuboresha miundombinu Dar es Salaam
Habari Mchanganyiko

Benki ya dunia yamwaga Sh. 800 bilioni kuboresha miundombinu Dar es Salaam

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam
Spread the love
SERIKALI ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB), wamejifunga kwenye mkataba wa utekelezaji awamu ya pili ya uboreshaji wa miundo mbinu jijini Dar es Salaam (DMDP 2), utakaogharimu takribani Sh. 800 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika hafla hiyo, mratibu wa miradi ya WB ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na

Wakala wa Barabara Vijijini – The Rural and Urban Roads Agency (Tarura), Mhandisi Humphrey Kanyenye, ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika katika awamu ya pili ya mradi.

Alisema, “katika jitihada za kuboresha miundombinu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Serikali imetia saini mradi wa uendelezaji wa jiji hilo kwa awamu ya pili ambapo utagharimu takribani Sh. 800 biliioni.

“Fedha hizo zimewekewa kipaumbele kwenye miundombinu ya barabara, masoko na uondoshaji wa taka ngumu zinazozalishwa kwenye masoko.”

Akishuhudia utiaji saini huo, Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Angellah Kairuki, amewataka wakandarasi hao waliotia saini kutekeleza mradi kwa wakati.

Waziri Kairuki alisema, “tunategemea mtajifunza katika awamu ya kwanza, na sitegemei kuona makosa ya kwanza yanajirudia. Mjue mmekopa na tunatarajia kuwa mradi huu utaenda kwa wakati na utamalizika kwa wakati. Mtakapoenda kinyume, tutarudi kwenye mkataba unavyosema.”

Kwa mujibu wa serikali ya Tanzania, utekelezaji wa miradi hiyo, utarajiwa kuanza  Aprili mwaka kesho, ambapo asilimia 74 ya fedha zitatumika kukarabati barabara, mifereji, maeneo ya wazi, masoko, vituo vya mabasi, kurekebisha miundombinu ya taka ngumu na kujengea uwezo kwa halmashauri za jijini la Dar es Salaam.

Rekodi zilizopo jijini Dar es Salaam zinaonyesha kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo, ulitekelezwa katika halmashauri zote tano za jiji la Dar es Salaam, ambazo ni Kinondoni, Ubungo, Temeke, Ilala na Kigamboni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!