Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya TEMDO yaanza kuzalisha vifaa tiba, bilioni tatu kutumika
Afya

TEMDO yaanza kuzalisha vifaa tiba, bilioni tatu kutumika

Spread the love

KATIKA kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba nchini, Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo ya Temdo Tanzania (TEMDO) imeanzisha karakana ya kisasa kuzalisha vifaa tiba kwa ajili ya hospitali pamoja vituo vya afya hapa nchini. Anaripoti Safina Sarwatt, Arusha…(endelea).

Hayo yamejiri baada ya kipindi cha mwaka 2021/2022 taasisi hiyo kuwekeza zaidi ya Sh.tatu bilioni kwa ajili karakana ya kisasa ya kutengeneza vifaa tiba aina 17. Mpaka sasa vifaa tiba aina saba vimeanza kuzalishwa.

Mkurugenzi Temdo

Akizungumza jijini Arusha katika mkutano mkuu wa 37 wa jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania ALAT, Mkurugenzi wa TEMDO, Mhandisi Prof. Frederick Kahimba amesema taasisi hiyo inamalengo makuu matatu ikiwemo kufanya tafiti zitakazotoa suluhu ya changamoto kwenye jamii.

“Pia tunafanya mafunzo ya kihandisi kwa watu ambao wanafanya kazi ndani ya viwanda kwa ajili ya uendeshaji, usalama viwandani pamoja mambo mbalimbali yanayohusiana na uzalishaji,”amesema Prof.Kahimba.

Amesema kuwa TEMDO inatengeneza vifaa tiba kwa ajili hospitali nchini lengo ni kupunguza uingizwaji wa vifaa kutoka nje ya nchi pamoja na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

“Leo tumekuja kuonyesha vifaa tiba ambayo vinatengenezwa TEMDO pamoja na kutoa elimu kwa Wajumbe wa mkutano mkuu wa 37 wa jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania ALAT kwani wao ndiyo wasimamizi wakuu wa hospitali na viwanda hivyo tunaamini kwamba hawataagiza vifaa tiba kutoka nje ya nchi tena,”amesema.

Amesema tayari taasisi hiyo imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha kuwa inazalisha vifaa vya kutosha.

Amesema vifaa hivyo ni pamoja vitanda vya wodi ya wajawazito, stendi za kuwekea drip, vitanda vya wagonjwa kufanyiwa uchunguzi pamoja na vitanda vya wagonjwa wanaolazwa hospitalini.

Amesema karakana hiyo kwa sasa inauwezo wa kutengeneza vitanda zaidi ya 500 vya wajawazito na vitanda na vya wagonjwa wanaolazwa hospitalini.

“Taasisi yetu pia tunazalisha majokofu ya kuhifadhia maiti, pia tunatengeneza viteketeza taka za mahospitali, hivyo tunakaribisha wadau wa afya na wamiliki wa hospitali binafsi na Serikali kununua vifaa tiba katika taasisi hiyo,” amesema .

Amesema TEMDO  wametengeneza mashine za aina mbalimbali za kilimo, viwandani pamoja na kutoa elimu kwa wahandisi na mafundi uchundo nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!