Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mpango akemea viongozi wa dini kuburuzana mahakamani
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango akemea viongozi wa dini kuburuzana mahakamani

Spread the love

MAKAMU wa Rais  Dk. Philip Mpango amewataka viongozi wa dini nchini kuwa na utaratibu wa kusuluhisha migogoro yao wenyewe badala ya kuipeleka mahakamani.

Ameseme migogoro hiyo inapaswa kushughulikiwa na mabaraza ya maadil  ili kupunguza vitendo vya mmomonyoko wa maadili. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(ndelea).

 

Dk Mpango ametoa wito huo jana tarehe 7 Mei 2023 Jijiini Dodoma katika ibada ya kumweka wakfu Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-KKKT- Dayosisi ya Dodoma, Christian Ndossa ya kumuingiza kazini pamoja na msaidizi wa Askofu Mchungaji Stanley Tabulu.

Amesema kitendo cha viongozi hao kuburuzana mahakama sio mpango wa Mungu hasa ikizingatiwa wao ndio wanaotakiwa kusimamia maadili.

“Ni waombe viongozi wa madhehebu ya dini hakikisheni mnamaliza wenyewe migogoro badala ya kupelekana mahakamani mkinzingatia kuwa nyinyi ndiyo mnaosimamia maadili” amesema.

Naye Askofu Christian Ndossa baada ya kusimikwa na kupewa majukumu ya kuongoza Dayosisi Kanisa hilo la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Dodoma amewataka watanzania kutunza mazingira ikiwemo na upandaji wa miti kwenye maeneo mbalimbali ili kuistawisha Nchi ya Tanzania hususani katika mikoa yenye asili ya ukame kama vile Dodoma na Singida.

Amewataka Watanzania kutowaachia suala hilo la upandaji miti Serikali peke yake bali jukumu liwe kwa kila mwananchi ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Fredric Shoo akizungumza kwenye ibada hiyo amesema viongozi wa dini hukerwa na baadhi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakifanya ubadhirifu wa mali za umma na kulisababishia taifa hasara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!