Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwinyi: Tanzania inatambua umuhimu wa vyombo vya habari
Habari Mchanganyiko

Dk. Mwinyi: Tanzania inatambua umuhimu wa vyombo vya habari

Spread the love

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu Vyombo wa Habari, kwani kupitia vyombo hivyo wananchi wanapata taarifa mbalimbali za shughuli za Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar …(endelea).

Dk. Mwinyi amesema hayo jana tarehe 3 Mei 2023 Visiwani Zanzibar wakati wa kilele Miaka 30  ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika visiwani humo.

“Tanzania inatambua umuhimu wa vyombo vya habari, kupitia vyombo vya habari wananchi wamejua shughuli zinazofanywa na Serikali, vilevile kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo, kama vile masuala ya kilimo na shughuli nyingine za kujikwamua kiuchumi,” amesema Dk. Mwinyi.

Ameendelea kusema kuwa, vyombo habari vimewasaidia wanasiasa, kutangaza sera za vyama vyao kwa wananchi, hivyo kufahamu mipango mbalimbali ya vyama vya siasa pamoja.

Aidha, Dk. Mwinyi ametoa wito kwa waandishi wa habari kuwa wazalendo na nchi yao kwani hakuna Uhuru usio na mipaka, wala  uhuru usio na wajibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!