RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu Vyombo wa Habari, kwani kupitia vyombo hivyo wananchi wanapata taarifa mbalimbali za shughuli za Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar …(endelea).
Dk. Mwinyi amesema hayo jana tarehe 3 Mei 2023 Visiwani Zanzibar wakati wa kilele Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika visiwani humo.
“Tanzania inatambua umuhimu wa vyombo vya habari, kupitia vyombo vya habari wananchi wamejua shughuli zinazofanywa na Serikali, vilevile kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo, kama vile masuala ya kilimo na shughuli nyingine za kujikwamua kiuchumi,” amesema Dk. Mwinyi.
Ameendelea kusema kuwa, vyombo habari vimewasaidia wanasiasa, kutangaza sera za vyama vyao kwa wananchi, hivyo kufahamu mipango mbalimbali ya vyama vya siasa pamoja.
Aidha, Dk. Mwinyi ametoa wito kwa waandishi wa habari kuwa wazalendo na nchi yao kwani hakuna Uhuru usio na mipaka, wala uhuru usio na wajibu.
Leave a comment