Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko UN yaipongeza Tanzania kuimarisha uhuru vyombo vya habari
Habari Mchanganyiko

UN yaipongeza Tanzania kuimarisha uhuru vyombo vya habari

Spread the love

UMOJA wa Mataifa umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini licha ya kukosolewa vikali na baadhi ya Watanzania wanaodai kwamba uhuru huo unatumika kueneza ushoga na usagaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar …(endelea).

Akizungumza jana tarehe 3 Mei 2023 mjini Zanzibar katika maadhinisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic amesema uhuru wa vyombo vya habari ni kichocheo cha kuimarisha haki nyingine.

“UN nchini Tanzania inatambua hitaji hili na itaendelea kushirikiana na Serikali, washirika, na vyombo vya habari ili kuimarisha upatikanaji wa habari kwa manufaa ya umma.

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua inazoendelea kufanya katika kufungua na kuimarisha vyombo vya habari,” ameeleza Zlatan.

Sherehe za miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani imeadhimishwa kitaifa mjini Zanzibar huku Bara la Afrika likiadhimisha siku hiyo nchini Zambia.

Kimataifa, siku hii imeadhimishwa jijini New York katika tukio maalum lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Kauli ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mwaka huu ni “Kuunda mustakbali wa haki: uhuru wa kujieleza kama chachu ya haki zote za binadamu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!