Tuesday , 14 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Miaka 59 ya Muungano imekuwa ya umoja, amani
Habari za Siasa

Rais Samia: Miaka 59 ya Muungano imekuwa ya umoja, amani

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema miaka 59 ya Muungano imekuwa yenye umoja, amani na ustawi wa Taifa kama ilivyokuwa ndoto za waasisi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Rais Samia ametoa ujumbe huo leo Jumatano tarehe 26 Aprili 2023 wakati Tanzania ikiadhimia miaka 59 ya muungano tangu kuasisiwa kwake mwaka 1964 na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere pamoja na Mzee Abeid Amani Karume.

Kupitia mtandao wa Twitter, Rais Samia amendika hivi; “Nawatakia nyote kheri tunapoadhimisha Miaka 59 ya Muungano. Imekuwa miaka 59 ya Umoja, yenye Amani na Ustawi, kama ilivyokuwa ndoto ya waasisi wetu, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Tuendelee kuidumisha tunu hii adhimu na ya kipekee kwa Taifa letu.”

Maadhimisho hayo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, safari hii yanafanyika kimkoa kama ambavyo Rais Samia alivyoagiza kwamba yafanyike katika ngazi ya mikoa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Tarehe 15 Aprili 2023 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jumamosi wakati alizindua Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Zanzibar, alisema Rais Dkt. Samia ameelekeza shughuli za maadhimisho hayo zifanyike kuanzia tarehe 17 Aprili, 2023 hadi siku ya kilele tarehe 26 Aprili, 2023.

Alisema kuwa maadhimisho hayo ambayo yatafanyika kupitia mikoa, taasisi za serikali na vyombo vyote vya ulinzi na usalama yaambatane na uzinduzi wa miradi ya maendeleo, shughuli za kijamii hususan upandaji miti, usafi wa mazingira na mashindano ya michezo na sanaa mbalimbali.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Habari za Siasa

Bunge lakemea utoroshwaji mifugo kuelekea Kenya

Spread the loveKamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na...

Habari za Siasa

CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo

Spread the loveCHAMA cha Wananchi (CUF), kimejipanga kujijenga kisiasa kuelekea chaguzi zijazo...

error: Content is protected !!