Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Miili ya waliojiua kwa njaa wakitaka kukutana na Yesu yafukuliwa
Kimataifa

Miili ya waliojiua kwa njaa wakitaka kukutana na Yesu yafukuliwa

Spread the love

 

POLISI nchini Kenya kwamba wamefukua miili ya watu watatu inayodhaniwa kuwa ya wafuasi wa dhehebu la kidini wanaoaminika walijiua kwa njaa, mashariki mwa nchi hiyo ili kukutana na Yesu.
Polisi imefukua miili hiyo juzi tarehe 21 Aprili ili kuifanyia uchunguzi zaidi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai katika wilaya ya Malindi, Charles Kamau alisema mchakato wa kufukua miili bado unaendelea na mpaka sasa maiti tatu zimepatikana.

Alisema maiti hizo hazijatambuliwa na chanzo cha vifo vyao hakijajulikana.

Makenzie Nthenge, ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Good News International, alijisalimisha kwa polisi na kufunguliwa mashtaka mwezi uliopita kufuatia vifo vya watoto wawili waliokufa kwa njaa wakiwa mikononi mwa wazazi wao.

Baadaye kiongozi huyo aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000 za Kenya.

Polisi waliripoti kukamatwa kwake Jumamosi iliyopita baada ya kugundua miili ya wafuasi wanne ambao inasemekana aliwaambia wasile ili wakutane na Yesu.

Wafuasi wengine 11 wa kanisa hilo – mmoja wao mdogo zaidi mwenye umri wa miaka 17 — walipelekwa hospitali, watatu kati yao wakiwa mahututi, baada ya kuokolewa wiki moja iliyopita pale maiti za mwanzo zilipogunduliwa kwenye msitu uliopo nje ya mji wa Malindi ulioko pwani ya mashariki.

Kamau alisema miili iliyopatikana hivi karibuni pia ilikuwa katika msitu wa Shakahola kufuatia uchunguzi wa kina katika eneo linalodhaniwa kuwa na kaburi la halaiki.

Polisi walivamia msitu huo baada ya kupata taarifa za vifo vya ‘wananchi wajinga’ wanaokufa kwa njaa kwa kisingizio cha kukutana na Yesu baada ya kulaghaiwa na Nthenge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!