Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yatuma salamu kwa wapinzani Uchaguzi Serikali za Mitaa
Habari za Siasa

CCM yatuma salamu kwa wapinzani Uchaguzi Serikali za Mitaa

Spread the love

 

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sophia Mjema, amesema hakuna chama cha siasa cha upinzani kitakachosumbua chama chake kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mjema ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Februari 2023, kupitia ukurasa wake wa Instergram, akizungumzia ziara yake ya kikazi ya siku mbili, aliyofanya mkoani Shinyanga.

Mwenezi huyo wa CCM amesema kuwa, chama chake kitachaguliwa na wananchi kutokana na weledi wa kazi inazofanya kupitia Serikali yake inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Jana tarehe 14 Februari 2023, nimewasili mkoani Shinyanga nikiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili. Nikizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya mkoa na Wilaya nimesisitiza kuwa hakuna chama chochote kitakachoisumbua CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu,” ameandika Mjema na kuongeza:

“Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wana wajibu wa kujibu hoja mbalimbali kwa vitendo na ushahidi kamili kwani kufanya hivyo itaondoa majungu. Nimesisitiza kuwa viongozi hao wana wajibu wa kufanya kazi ya kutangaza sera za CCM na Ilani yake hivyo kupitia mikutano mbalimbali ya kuimarisha chama wanapaswa kueleza mafanikio ya serikali.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!