Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa AAFP yamkumbuka Hayati Magufuli, wampa neno Rais Samia
Habari za Siasa

AAFP yamkumbuka Hayati Magufuli, wampa neno Rais Samia

Spread the love

CHAMA cha Wakulima nchini (AAFP), kimesema kinamkumbuka aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, kutokana na kazi kubwa aliyofanya kulinda demokrasia na kuwainua wakulima kwa kuondoa utitiri wa kodi zilizokuwa zinawakandamiza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili, tarehe 12 Februari 2023, na Mwenyekiti wa AAFP anayemaliza muda wake, Said Soud Said, katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Nafungua mkutano huu kwa kumkumbuka hayati Magufuli, kutokana na uwanja wa demokrasia ambao kwa namna moja au nyingine aliwezssha kifikia hatua ya Tanzania kuwa nchi ya amani na utulivu,” amesema Said.

Mwenyekiti huyo wa AAFP, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuendeleza yale mema yaliyoachwa na mtangulizi wake aliyefariki Dunia Machi 2021.

“Magufuli kutokana na uwezo wake kisiasa aliwafanya wakulima wa nchi hii waendelee kulima kokote wanakotaka na wauze mazao yao kokote. Tunataka Rais Samia aliyekamata kijiti chake aendelee kulinda demokrasia na hatimaye kufanya Tanzania kuishi kwa amani na utulivu.”

AAFP kinafanya mkutano wake mkuu uliobeba ajenda mbalimbali ikiwemo kujadili na kupitisha sera yake ya jinsia, kufanya marekebisho madogo ya katiba na kanuni zake.

Masuala mengine ni kuwasilisha na kuidhinisha taarifa ya utekelezaji ya 2028 hadi 2023 na uchaguzi wa viongozi kitaifa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!