Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yafichua madhila wanayopitia vijana wa Dar
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yafichua madhila wanayopitia vijana wa Dar

Spread the love

NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, kimeiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto za uhaba wa ajira jijini humo, ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi yao wasiokuwa na vyanzo vya mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ombi hilo limetolewa leo tarehe 10 Februari 2023 na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Dar es Salaam, Felix Kamugisha, akizungumza na MwanaHALISI Online, kwa njia ya simu.

“Vijana wa Dar es Salaam wengi hawana ajira, Dar es Salaam ndiyo jiji kitovu cha uchumi wa nchi yetu. Kimbilio la vijana wengi wa Tanzania ni Dar es Salaam kwa kuwa wanaamini hapa ni mahali sahihi kwao lakini wanapoingia hukuta mambo tofauti sana,hali ngumu sana,” amesema Kamugisha.

Mwenyekiti huyo amesema, ugumu wa maisha unaotokana na ukosefu wa ajira unaowakabili vijana wengi wa jiji hilo, umesababisha baadhi yao kuingia katika shughuli haramu, ikiwemo biashara ya ngono na wizi.

“Ukienda Kimboka pale Buguruni usiku utawakuta watoto wadogo wanauza miili yao, Serikali ipo inatazama. Tandika pana mtaa una nyumba zaidi ya 100 wanauza miili yao wenyeviti na askari kata wanachukua kodi pamoja na kuvilinda na kulea vikundi hivyo,” amesema Kamugisha.

Mbali na changamoto zinazowakabili wasiokuwa na ajira, Kamugisha amedai hata baadhi ya vijana wenye ajira wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kupewa mishahara midogo, kutopewa mikataba ya ajira.

“Dar es Salaam ndiyo jiji lenye viwanda vingi hapa nchini lakini vijana wengi waliopo viwandani hawapati haki zao, ni mateso na unyanyasaji wa kijinsia. Kule viwandani maafisa rasilimali watu ndiyo miungu watu anaweza kutembea kimapenzi na mdada yeyote hata kama hataki, wanatumia nafasi zao kuvunja utu wa mtu,” amesema Kamugisha.

Mwenyekiti huyo wa Vijana Dar es Salaam kupitia ACT-Wazalendo, amedai kwamba “mishahara haiendani na kazi wanazofanya, mfano kuna kiwanda kimoja mhandisi wa kihindi analipwa milioni nne, wakati wa kitanzania analipwa laki tatu ilhali wanafanya kazi moja na wote wana sifa za kitaaluma.

Wakati huo huo, Kamugisha amesema kuwa, mikopo inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya vijana haiwafikii wahusika wengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!