Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mawakili: Kikao kilichomng’oa Mbatia, wenzie ni halali
Habari Mchanganyiko

Mawakili: Kikao kilichomng’oa Mbatia, wenzie ni halali

Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, Mohamedi Tibanyendera.
Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imeelezwa kuwa, kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, kilichomuondoa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia na wenzake, kilikuwa halali na kwamba uamuzi huo ulipewa baraka na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Madai hayo yalitolewa Leo tarehe 25 Januari 2023 na mawakili wa wajibu maombi  katika kesi Na. 570/2023, iliyofunguliwa na wajumbe wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya NCCR-Mageuzi, kupinga uteuzi wao kutenguliwa kinyume Cha sheria.

Ni wakati wanajibu hoja za mawakili wa wajumbe hao wa zamani (waleta maombi), walizotoa jana Jumanne mahakamani hapo, kupinga uteuzi wa wajumbe wapya (wajibu maombi).

Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa mahakamani hapo jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Ephery Kisanya.

Akijibu hoja ya mawakili wa waleta maombi kwamba kikao cha halmashauri hiyo kilichofanyika tarehe 21 Mei 2022, chini ya Joseph Selasini, kilikuwa batili Kwa kuwa kiliahirishwa Hadi Septemba 2022 na kikao Cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi, cha tarehe 15 Mei 2022.

Mwakilishi wa mjibu maombi namba sita, Faustine Sungura, amedai Msajili wa Vyama vya Siasa alithibitisha uhalali wa kikao hicho pamoja na maamuzi yake ya kuwaondoa wajumbe wa zamani wa bodi hiyo pamoja na baadhi ya viongozi, kupitia barua yake aliyoandika tarehe 25 Mei mwaka jana.

Naye Wakili wa mjibu maombi namba moja hadi tano, Novatus Mhangwa, amedai kwamba mchakato wa kuwaondoa wajumbe hao kama wadhamini wa NCCR-Mageuzi, ulikuwa halali kwa madai kwamba mabadiliko hayo yalithibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

Akijibu hoja ya waleta maombi iliyodai kwamba wajumbe wa zamani waliondolewa kinyume Cha Sheria na watu ambao baadae walijiteua kushika nafasi zao, Wakili Mhangwa amedai uteuzi huo ulifanywa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi. Hata hivyo, wadhamini hao wapya pia walishiriki kikao hicho kama sehemu ya wajumbe.

Jaji Kisanya ameahirisha kesi hiyo Kwa muda, Hadi saa 9.00 mchana Kwa ajili ya mawakili wa waleta maombi kujibu hoja hizo zilizotolewa na mawakili wa wajibu maombi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!