Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Waziri Gwajima atua NMB, atoa ujumbe kwa makundi maalum
Habari Mchanganyiko

Waziri Gwajima atua NMB, atoa ujumbe kwa makundi maalum

Spread the love

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima, ametembelea Makao Makuu ya Benki ya NMB na kuipongeza Menejimenti na wafanyakazi kwa mafanikio yaliyowapa Tuzo 22 mwaka jana. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pia, waziri huyo amekikiri taasisi hiyo imebeba fursa nyingi na kuyataka Makundi Maalum kuzichangamkia Ili kukua kiuchumi.

Waziri wa maendeleo ya Jamii, jinsia wanawake na makundi Maalum, Dkt Doroth Gwajima(katikati) akiteta jambo na Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna(Kushoto) alipotembelea makao makuu ya Benki ya NMB kwaajili ya kujua utendaji kazi wa Benki ya NMB. Kulia ni Afisa mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori.

Dk Gwajima alifanya ziara hiyo jana Jumanne tarehe 24 Januari 2023, ambako alipokelewa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa NMB, Ruth Zaipuna na Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo, Juma Kimori.

Alisema pamoja na mambo mengine, alitembelea hapo ili kujua fursa ilizonazo taasisi hiyo Ili aweze kuzizungumzia mbele ya Jamii, hususani Makundi Maalum yaliyo chini ya wizara yake.

Waziri Gwajima alibainisha licha ya kutambua ukubwa na ukongwe wa NMB, lakini amevutiwa zaidi na uwekezaji wa kiteknolojia na ubunifu wa suluhu za kihuduma, mambo yaliyochangia jamii kuhudumiwa kwa wepesi na urahisi wakiwa mbali na matawi ya benki hiyo.

“Teknolojia na bunifu zenu zimetuweka mbali na matawi ya benki yenu. Hongera sana kwenu kwa kurahisisha huduma za kibeki, na mmestahili tuzo mlizotwaa mwaka jana, ambao mmenyakua zaidi ya tuzo 20 za kitaifa na kimataifa. Tuzo hizo zimebeba ujumbe mkubwa na muhimu kwa Watanzania wa kada zote,” alisema.

“Nimejifunza mengi kupitia ziara hii na nimepata somo kubwa la kuwaambia Wana Jamii, hususani Makundi Maalum yaliyo chini ya wizara yangu. Wenye uhitaji wa fursa hizi wako mengi, ila hawajui wapi wanakoweza kuzipata. Nitkuwa balozi mwema wa NMB,” alisema Dk Gwajima.

 

Alibainisha, NMB imetoa mchango mkubwa kwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuiwezesha kutekeleza Programu ya Uwezeshaji kwa Makundi Maalum Kiuchumi, huku akiyataka makundi kama Machinga, Bodaboda na mengineyo yaende na kasi ya NMB Kidijitali, hasa ukizingatia huduma zao zimesambaa kote nchini.

Mwaka 2022, ulikuwa wa mafanikio kwa NMB, baada ya taasisi hiyo kinara ya fedha nchini kunyakua zaidi ya tuzo 20, zikiwemo za kimataifa kutoka taasisi na majarida kama Global Brands Magazine, World Economic International Business, Global Banking Finance, International Bankers, IFC, Employer Branding Institute na Euro Money na zile za kitaifa kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Awali, CEO Zaipuna aliwaambia wana habari kwamba wameitumia ziara hiyo kumueleza Waziri Gwajima ukubwa was fursa walizonazo kwa makundi maalum yaliyo chini ya wizara yake na kwamba NMB imejikita vya kutosha katika uwekezaji wa kiteknolojia na ubunifu.

Alibainisha kwamba suluhu hizo za kihuduma zimelenga kurahisisha huduma za kifedha miongoni mwa Watanzania, ambao wametanuliwa wigo huo kiasi cha kuwawezesha kufungua akaunti, kufanya miamala na hata kukopa pesa kwa njia ya simu bila kufika kwenye matawi yao.

“Yote hayo yanaweza kufanywa na mteja wetu kupitia Teleza Kidigitali, Mwamvuli wenye huduma chanya na rafiki kibao, zilizolenga na kufanikisha kuzirasmisha Sekta zisizo rasmi na kuwajumuisha Watanzania katika huduma za kifedha,” alifanya Zaipuna, ambaye alikuwa na Mwaka Bora wa 2022 kiutendaji akitunukiwa tuzo kadhaa kitaifa na kimataifa.

Aliyataka Makundi Maalum yakiwemo ya wanawake na vijana, kuzitumia vema fursa walizonazo NMB kujinyanyua kiuchumi na kibiashara Ili kukuza mitaji, mapato yao na kuchangia ukuaji kiuchumi wa taifa kupitia kodi na tozo nyinginezo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!