Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali kufanya utafiti wa hali ya umasikini
Habari Mchanganyiko

Serikali kufanya utafiti wa hali ya umasikini

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania ipo katika maandalizi ya mwisho ya kufanya utafiti wa hali ya umasikini nchini kwa mwaka 2023/2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 18 Januari 2023 na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa, katika kikao kazi cha kujadili hali ya mfumuko wa bei.

“Tunategemea kufanya utafiti kwenye mapato na matumizi ya kaya ambayo itatupa hali ya umasikini, tunafanya maandalizi ya mwisho ya kufanya utafiti,” amesema Dk. Chuwa.

Mtakwimu huyo wa Serikali amesema utafiti wa mwisho wa hali ya umasikini ulifanyika 2017/18, ambapo ulionyesha asilimia 28.2 ya wananchi wanaishi chini ya mstari wa umasikini.

Kuhusu Pato la Taifa (GDP), Dk. Chuwa amesema maoteo ya ukuaji wake ni asilimia 5.3, kutokana na majanga yanayoendelea kutokea duniani, hususan athari za vita kati ya Urusi na Ukraine.

“Maoteo tuliyofanya yalituonyesha GDP itakuwa kwa asilimia 5.3 katika robo ya mwaka, lakini tuna sera ya kufanya marejeo kulingana na global crisis ambapo tumepata maoteo ya asilimia 5.2 lakini Machi 2023 tutajua kama tumebaki kwenye maoteo yaleyale,” amesema Dk. Chuwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!