Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko NBS yatabiri mfumuko wa bei kupungua
Habari Mchanganyiko

NBS yatabiri mfumuko wa bei kupungua

Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Dk. Albina Chuwa
Spread the love

 

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetabiri kupungua kwa mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi, kutoka asilimia 9.7, kufikia Machi mwaka huu.  Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo 18 Januari 2023, Dk. Albina Chuwa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, amedai tofauti na ilivyokuwa Desemba mwaka jana, katika kipindi cha robo mwaka ya kwanza ya 2023 (Januari hadi Machi), mfumuko huo, utapungua hadi kufikia 8.4 asilimia.

Dk. Chuwa alitoa kauli hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika kilichoitwa, “kikao kazi cha idara yake.”

Alisema, bei hizo zitapungua kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali kudhibiti mfumuko wake, ikiwemo kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuongeza bajeti na kutoa ruzuku kwenye mafuta na mbolea.

Akijibu baadhi ya maswali ya waandishi waliotaka kufahamu vigezo vinavyotumika kupima mfumuko huo wa bei, Dk. Chuwa alisema, tofauti zinatokana na taratibu zinazopima viashiria hivyo.

Alisema, tofauti hiyo inatokana na NBS kufanya takwimu zake kwa kuangalia bei za bidhaa za nchi nzima kisha hutoa wastani wa mfumuko wa bei kitaifa.

Baadhi ya waandishi walitaka kufahamu vigezo vinavyotumniwa na taasisi hiyo, kufuatia madai kuwa ripoti ya NBS mara nyingi huonyesha tofauti na uhalisia.

Baadhi ya mifano iliyotolewa, ni kwamba wakati NBS wanasema mfumuko wa bei kitaifa umepungua, bei za bidhaa hasa vyakula, zinaonekana kuwa juu nchi mzima.

Ametolea mfano wa bei ya mchele nchini ambapo katika baadhi ya mikoa, huuzwa kati ya Sh. 2,500 na 3,000; na au hadi 3,500, lakini wastani wake kitaifa ni 2,500 kwa kilo.

“Bei ya michele tunapima wastani wake kwa kilo ya kwa nchi, tunachukua wastani wa bei za mikoa yote ya Tanzania Bara, kisha tunafanya wastani wa bei kwa nchi. Hapo utakuta ile bei ya Sh. 3,000 na 2,000 wastani wake inakuwa Sh. 2,500,” ameeleza.

Akizungumzia ustahamilivu wa mfumuko wa bei, Dk. Chuwa alisema, mfumuko huo uko stahimilivu, kwa kuwa bado umebaki kwenye tarakimu moja ambapo kwa mwaka 2022 ulikuwa 4.3 asilimia.

Katika hatua nyingine, Dk. Chuwa amezungumzia fahirisi ya bei za bidhaa, akisema kati ya Sh. 100 ya mwananchi, asilimia 28.2 hutumika kwa bidhaa za vyakula na vinywaji, wakati asilimia 15 zinakwenda kwenye nishati ikiwemo umeme, gesi na mafuta.

Amesema, asilimia 14 kati ya Sh. 100 ya mwananchi inakwenda katika usafiri.

Alisema, pamoja na kuonekana bei za bidhaa hasa vyakula kuonekana kupanda mtaani mwezi Desemba 2022, lakini mfumuko wa bei kitaifa ulishuka hadi kufikia asilimia 4.8, kutoka asilimia 4.9, iliyokuwa Novemba.

Aliongeza, “tumepima viwango hivyo kwa kuangalia mapato na matukizi ya kaya. Serikali imejipanga kupungua gharama za uzalishaji mazao ya kilimo, ili kuongeza kipato cha mwananchi kwa kuwa tunafahamu kilimo ni nguvu kazi ya taifa.”

Kwa mujibu wa Dk. Chuwa, mfumuko wa bei kitaifa kwa Desemba ulipungua kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa zisizokuwa za vyakula, ikiwemo dizeli na petroli.

Alisema, bei ya saruji ilipungua kutoka asilimia 3.2 hadi 2.5, gesi ya kupikia (asilimia 13.8 hadi 11.8).

Hata hivyo, Dk. Chuwa amesema, serikali iko katika maandalizi ya mwisho ya kufanya utafiti wa hali ya umasikini nchini kwa mwaka wa 2023/2024.

“…tunategemea kufanya utafuti kwenye mapato na matumizi ya kaya, ambayo itatupa hali ya umasikini. Tuko kwenye maandalizi ya mwisho ya kufanya hivyo,” alieleza.

Mtakwimu huyo wa serikali amesema, utafiti wa mwisho wa hali ya umasikini ulifanyika mwaka 2017/18, ambapo ulionyesha asilimia 28.2 ya wananchi, wanaishi chini ya mstari wa umasikini.

Lakini wakati serikali ya Tanzania, ikieleza kuwa mfumuko wa bei unatarajiwa kuhuka kufikia Machi mwaka huu, Benki ya Dunia (WB), inaendelea kusisitiza kuwa “dunia iko karibu na mdororo wa uchumi.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Washington DC, nchini Marekani, Rais wa WB, David Malpass amesema, baadhi ya nchi tayari zimepandisha viwango vyao vya riba na huenda sasa zinafikia hatua ambayo hazihitaji kuongeza.

Kwa mujibu wa benki hiyo, mfumuko wa bei ulimwenguni utazidi kuongezeka, huku ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2023 ukishuka kutoka asilimia 3 hadi 1.9 asilimia.

Kuhusu pato la Taifa (GDP), Dk. Chuwa amesema, matokeo ya ukuaji wake ni asilimia 5.3, kutokana na majanga yanayoendelea kutokea duniani, hususan athari za vita kati ya Urusi na Ukraine.

“Matokeo tuliyofanya yalituonyesha GDP itakuwa kwa asilimia 5.3 katika robo ya mwaka, lakini tuna sera ya kufanya marejeo kulingana na global crisis ambapo tumepata maotekeo ya asilimia 5.2, lakini Machi 2023 tutajua kama tumebaki kwenye matokeo yaleyale,” alisisitiza.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!