Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgeja ataka vyama visitumie mikutano ya hadhara kuchafua wengine
Habari Mchanganyiko

Mgeja ataka vyama visitumie mikutano ya hadhara kuchafua wengine

Spread the love

MWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo foundation Khamis Mgeja amevitaka vyama vya siasa nchini kutumia ruhusa ya Mikutano ya hadhara iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuelezea mazuri yaliyofanywa na serikali yao pamoja na kunadi sera za vyama vyao na siyo kutumia vibaya ruhusa hiyo kuchafua vyama vingine. Anaripoti Paul Kayanda, Kahama…(endelea).

Mgeja ametoa kauli hiyo Kahama mkoani Shinyanga wakati akizungumza na MwanaHalisi Online kuhusu tamko la kuruhusu mikutano ya hadhara kwa wananchi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema nia ya Rais ni njema na isitumike vibaya kuchafua taswira ya chama kimoja badala ya kuhubiri maziri yaliyo fanyika.

Mgeja amesema kama mwanademokrasia hatua hiyo ni ya kumpongezwa kwani Rais ameonyesha kwa vitendo kwamba yeye ni mwanademokrasia wa kweli.

“Hili ni jambo la msingi sana kwetu na pia litakuwa na faida za msingi na kwa mantiki hiyo basi suala la ruhusa ni jambo moja lakini jambo la pili ni matumizi ya hiyo ruhusa kwa vyama vya siasa vya nchi yetu,” alisema Mgeja.

Aidha Mgeja alitumia fursa hiyo kuviomba vyama vya siasa nchini kikiwemo chama tawala kwamba vyote vimeruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara siyo vyama pinzani peke yake, kwa maana hiyo uwepo utaratibu wa kushindana kwa hoja na kwani vyama hivi siyo uadui.

Alivitaka kutotunishiana misuli pindi vinapokwenda kwenye majukwaa huko kwa wananchi na kuongeza kuwa kama watanzania wazalendo hawatapenda kuona kejeli na matusi badala yake siasa ziwe za kuelezeana mazuri na mikakati yao watakayofanya kwa kuleta maendeleo kwa wananchi.

Pia alihimiza kuwepo na agenda moja ya kitafia wakati wanapokuwa majukwaani hasa suala la amani kwani bila amani hakuna siasa safi wala maendeleo badala yake kutakuwepo minyukano ambayo ni kiashirio cha kuvunja amani yetu.

Pamoja na mambo mengine aliiomba serikali kupitia wizara ya kilimo isogeze mawakala wa pembejeo karibu na maeneo ya wakulima ili wasaidie kusogeza huduma za pembejeo .

Amesema baadhi ya maeneo ya wakulima wanatembea umbali mrefu wa kilometa 30 mpaka 60 kufuata huduma hiyo.

Aidha, naye mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM tawi la Sango Kata ya Nyasubi, Charles Lubala alisema nje ya siasa kuna kilimo hasa ikizingatiwa siasa na kilimo vinakwenda pamoja hivyo wakulima wasikate tamaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!