Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari Mamlaka za Mabonde ya maji zaagizwa kubomoa matuta yanayochepusha mito
HabariTangulizi

Mamlaka za Mabonde ya maji zaagizwa kubomoa matuta yanayochepusha mito

Spread the love

MAMLAKA za Mabonde ya Maji nchini, zimeagizwa kuanza mara moja ubomoaji wa matuta yaliyojengwa kwaajili ya kuchepusha maji ya mito kwenda kwenye mashamba bila vibali. Anaripoti Mwandishi Wetu Iringa…(endelea).

Pia Dk. Mpango ameagiza kupelekewa vibali vyote vilivyotolewa kwa watumiaji wa maji ya mito.

Ametoa maagizo hayo leo tarehe 19 Septemba, 2022 katika kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vyama maji lililoandaliwa na Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA).

“Viongozi wa mamlaka ya mabonde ya maji nawataka kuchukua hatua sasa, chukueni hatua leo, wale walioziba mto Ruaha bila vibali sahihi vya matumizi ya maji bomoeni na mbomoe kwa gharama zao na wale wenye vibali nataka kuviona hivyo vibali,” amesema Dk. Mpango.

Makamu wa Rais ameitaka Wizara kutekeleza maagizo yake ya kufanya tathimini ya matumizi ya maji na apewe ripoti hiyo haraka.

“Wizara nilishasema mfanye tathimni ya matumizi ya maji, lakini kuniambia hata mmefika wapi hataki kuniambia sijui mnataka kumwambia nani kwasababu lazima tujue hii mito na maziwa yetu ina maji kiasi gani hii mifereji inachukua maji kiasi gani na yanarudi kiasi gani,” amesema Dk. Mpango.

Pia ameiagiza Wizara ya Mifugo kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kufanya tathimini ya mifugo kutafuta eneo la kuihamishia na kuanza kufuga kisasa,” amesema.

Amesema anaamini vita hiyo ni kubwa lakini amewahakikishia watanzania kuwa wataishinda vita hivyo.

“Hii vita ni kubwa sikuianza vita hii nikijua ni ndogo, najua vita ni kubwa lakini tutashinda, kwahiyo hata hao ambao wanasemekana wanatengeneza namna mahakamani kuzuia minada, tutazungumza na mihimili hiyo kwasababu kilicho kinyume na mihimili hakikubaliki,” amesema Dk. Mpango.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!