Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apangua, ateua makatibu wakuu
Habari za Siasa

Rais Samia apangua, ateua makatibu wakuu

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 14 Disemba, 2022 ameteua makatibu wakuu wa wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda pamoja na wizara ya mambo ya ndani ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Hashil Twaib Abdalah

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jijini Washington nchini Marekani, uteuzi huo umeanza tarehe 9 Disemba, 2022.

Makatibu wakuu walioteuliwa ni pamoja na kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Hashil Twaib Abdalah. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Kaspar Kaspar Mmuya

Pia amemteua Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Rais Samia yupo nchini Marekani kushiriki mkutano wa viongozi wa Afrika ambao unafanyika kwa muda wa siku tatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!