Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwandishi wa Habari TBC afariki akishuka mlima Kilimanjaro
Habari Mchanganyiko

Mwandishi wa Habari TBC afariki akishuka mlima Kilimanjaro

Spread the love

MWANDISHI wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Manyara Joachim Kapembe amefariki dunia alipokuwa akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Disemba, 2022 na Shirika hilo, Kapembe amefariki jana tarehe 13 Disemba, 2022.

Imesema Kapembe pamoja na watendaji wengine wa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari walipanda kwenye mlima Kilimanjaro tarehe 9 Disemba, 2022 kwa ajili uzinduzi wa intaneti ya mwendokasi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Mwandishi huyo, alizaliwa tarehe 26 Februari mwaka 1977 wilayani Muheza mkoani Tanga.

Aliajiriwa na TBC Oktoba Mosi mwaka 2011 kwa cheo cha mpiga picha daraja la II.

Hadi anafariki dunia tarehe 13 mwezi huu alikuwa na cheo cha mpiga picha mkuu daraja la I.

Joachim Kapembe ameacha mke na watoto wawili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!