Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Tax awaasa vijana kuiga falsafa za uongozi wa Nyerere
Habari Mchanganyiko

Dk. Tax awaasa vijana kuiga falsafa za uongozi wa Nyerere

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax amewaasa vijana kutumia vyema Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kujifunza, kubadilishana mawazo juu ya falsafa za Mwalimu Nyerere pamoja na kuimarisha amani na umoja katika jamii.

Dk. Tax ametoa wito huo alipokuwa akifungua mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa kundi la kwanza la viongozi vijana 60 kutoka nchi zaidi ya 40 Barani Afrika jana tarehe 25 Novemba, 2022 Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Tax aliwasisitiza vijana hao kutumia mafunzo hayo kuinufaisha jamii inayowazunguka.

“Napenda kutumia fursa hii kuwasihi vijana wa kizazi kipya cha Viongozi wa Afrika na watu wa Afrika, kufanya kazi kwa umoja, ushirikiano, na imani thabiti, kwani bila kufanya hivyo ni vigumu kuwa na mustakabali wa Afrika tunayoitaka,” alisema Dk. Tax.

Dk. Tax aliongeza kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, imejipanga kuhakikisha vijana wanawezeshwa ili kuendeleza amani, usalama na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Dk. Stergomena Tax

“Katika kuenzi mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere katika kukuza umoja, amani na maendeleo ya watu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla, Serikali inaendelea kuunga mkono mipango ya amani kwa kuchangia Misheni za ulinzi wa amani Barani Afrika na Kikanda. Leo hii Tanzania ni nchi ya 13 kwa ushiriki katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa Duniani,” aliongeza Dk. Tax.

Bara la Afrika limebarikiwa rasilimali nyingi, tuchanganye maarifa, ujuzi wa uongozi, na maliasili ilizonazo ili kupeleka bara la Afrika katika ngazi za juu zaidi. Kwa kufanya hivyo, vijana mtakuwa mmeenzi falsafa za uongozi za Mwalimu Nyerere, aliyeongoza mapambano ya kupigania uhuru, umoja, na kujenga misingi imara ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Awali akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku alisema kuwa programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yanayotolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ni mpango unaolenga kushirikisha viongozi vijana katika kutoa mafunzo, changamoto, kufafanua na kubadilisha mtazamo wa kizazi kipya cha Afrika kuwa viongozi wanaowajibika, wanaojitolea na wapenda amani.

“Malengo ya taasisi yetu ni kutafiti na kueneza falsafa ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, amani, umoja na maendeleo ya watu. viongozi wazuri na wenye tija wa sasa na wa siku zijazo wa bara hili,” alisema Butiku.

Mafunzo hayo yametolewa kwa vijana 60 kutoka mataifa mbalimbali ambayo ni Botswana, Burundi, Cameroon, Djibouti, Misri, Ethiopia, Gabon, Guinea, Kenya, Libya, Liberia, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sudani, Sudani Kusini, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, na Zambia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

error: Content is protected !!