CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinafanya ziara barani Ulaya kwa ajili ya kutafuta uungwaji mkono na Jumuiya za Kimataifa katika msuala ya uimarishaji demokrasia nchini, upatikanaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema iliyotolewa Jana Jumamosi, ujumbe wa Chadema katika ziara hiyo unaongozwa na Makamu wake Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu, wengine ni Katibu Mkuu, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim.
“Ziara hiyo inahusisha nchi za Ujerumani na Ubelgiji ambapo ujumbe wa Chadema utawasilisha wito wa kuungwa mkono mpango wa kupatikana Kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, urudishwaji wa haki ya kufanya siasa ikiwemo mikutano ya hadhara,” imesema taarifa ya Mrema.
Taarifa ya Mrema imetaja taasisi ambazo ujumbe wa Chadema utawasilisha wito huo, ikiwemo Chama cha CDU, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Ushirikiano was Kiuchumi na Maendeleo Ujerumani, Bunge la Umoja wa Ulaya na Taasisi ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.
“Lengo ni kuhakikisha mazingira ya siasa Tanzania yanaimarika na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi zinapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 Ili kuhakikisha uwepo wa uchaguzi huru, haki na unaokubalika,” imesema taarifa ya Mrema.
Leave a comment