Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania kuzidi kunufaika na miradi ya Shirika la Miliki Bunifu Duniani
Habari Mchanganyiko

Tanzania kuzidi kunufaika na miradi ya Shirika la Miliki Bunifu Duniani

Spread the love

 

BALOZI na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Jijini Geneva Uswisi, Balozi Maimuna Tarishi amesema kuwa Tanzania inaendelea kunufaika na miradi mingi ambayo hutolewa na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa alipotembelea ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) jana tarehe 22 Novemba, 2022 ili kujionea namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake ambapo pia alipokea taarifa za utekelezaji wa shughuli na miradi inayofanyika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na WIPO, BRELA ikiwa ni msimamizi mkuu wa majukumu ya miliki ubunifu nchini.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Andrew Mkapa akimkaribisha katika ofisi za BRELA amebainisha majukumu ya Taasisi kisheria na namna ambavyo BRELA inashirikiana na WIPO kwa karibu kutokana na utekelezaji wa jukumu la miliki ubunifu nchini Tanzania.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu, Loy Mhando alimshukuru Balozi Tarishi kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia masuala ya Miliki Ubunifu na kuwa kiungo kati ya Tanzania na WIPO na kumueleza kuwa baada ya mkutano wa 63 wa WIPO uliofanyika mwezi Julai, 2022 Geneva-Uswisi, BRELA imeanza kutekeleza maeneo ya mashirikiano, hivyo kuiomba ofisi yake kutoa usaidizi wa karibu wa kufuatailia masuala yanayowasilishwa WIPO.

Mhando alibainisha maeneo yanayohitaji usaidizi kutoka ofisi yake ni pamoja na rasimu ya Sera ya Miliki Ubunifu ya Taifa kwa ajili ya kupata usaidizi wa kitaalamu ili kuboresha nyaraka hiyo kwa kuwa WIPO ni wabobezi wa masuala ya Miliki Ubunifu.

Vilevile, alimuomba anapokutana na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO kuwasilisha uhitaji kuwajengea uwezo watumishi na watumiaji wa Miliki Ubunifu ili waweze kusimamia na kutumia Miliki Ubunifu kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Aidha, alimueleza Balozi kuwa, Tanzania kupitia WIPO imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zinazofanyika kwa ushirikiano ikiwemo kuwezesha matumizi ya Miliki Ubunifu kwa wafanyabiashara na wabunifu; programu ya shahada ya uzamili inayotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kishirikiana na ARIPO, BRELA na WIPO na tathmini ya miliki ubunifu katika biashara; nk.

Mkapa amelimwomba Balozi Tarishi kuishirikisha BRELA katika fursa mbalimbali zinazojitokeza katika mashirika ya kimataifa kwani BRELA ipo tayari kushirikiana na Ofisi yake kikamilifu kwa ajili ya mafaniko ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

error: Content is protected !!