Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT hatarini kujiondoa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
Habari za SiasaTangulizi

ACT hatarini kujiondoa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

Spread the love

 

KAMATI maalum ya Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo upande wa Zanzibar, imeagiza Sekretarieti ya chama hicho kuratibu vikao vya viongozi na wanachama kwa ajili ya kutoa maelekezo yao juu ya mustakabali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na hali ya kisiasa visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa ACT-Wazalendo, Salim Bimani, kamati hiyo imetoa maelekezo hayo baada ya kuketi jana tarehe 15 Novemba 2022 visiwani Zanzibar, kujadili hali ya kisiasa iliyoibuka kufuatia hatua ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, kumteua Thabit Idarous Faina, kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Taarifa ya Bimani imeeleza kuwa, kamati hiyo imeagiza vikao hivyo baada ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani humo katika kipindi cha miaka miwili pamoja na uteuzi wa Faina, anayedaiwa kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2020.

“Kikao hicho cha dharura kimeitishwa kujadili hali ya kisiasa Zanzibar kutokana na taharuki ya kisiasa iliyoibuka kufuatia uteuzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC Ndugu Thabit Idarous Faina ambaye ndiye aliyesimamia Uchaguzi Mkuu wa 2020 uliosababisha mauaji na maafa makubwa katika nchi.

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

“Uteuzi huo ukiambatana na matukio mengine yasiyoridhisha katika kipindi cha miaka miwili iliopita umesababisha Wazanzibar kupoteza imani na kutilia shaka uwepo wa dhamira njema na nia ya dhati ya kujenga maridhiano ya kweli na umoja wa kitaifa kama ilivyokuwa imeahidiwa,” imesema taarifa ya Bimani na kuongeza:

“Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama upande wa Zanzibar baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa imeielekeza Sekretarieti ya Chama upande wa Zanzibar kuratibu vikao vya ndani vya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama kusikiliza na kutoa maelekezo yao juu ya mustakabali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hali ya kisiasa Zanzibar.

Kamati Maalum imesisitiza kwamba vikao hivyo vya ndani vya kusikiliza maoni ni utekelezaji wa ahadi ya uongozi wa Chama Taifa ya kusikiliza maoni na tathmini ya Wanachama baada ya Miaka miwili ya ujenzi wa Maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kamati Maalum imeagiza ripoti ya vikao hivyo iwasilishwe kwenye Kikao cha Kamati Kuu ya Chama.

1 Comment

  • Asante act.asante hizo nidalili za uwoga wapiga kula hawateuliwi na rais sasa uwoga wenye mashaka wanini kama uwoga ni mila tuache kwa sababu madhara yake nimakubwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!