December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Dk. Mwinyi ateua viongozi

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, leo Jumatano, tarehe 16 Novemba 2022, amefanya uteuzi wa viongozi wawili, akiwemo Dk. Sharifa Omar Salim, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said.

“Dk. Sharifa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma. Dk. Sharifa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),” imesema taarifa ya Mhandisi Zena.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiongozi mwingine aliyeteuliwa ni Dk. Hashim Hamza Chande, kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Kabla ya uteuzi huo, Dk. Hashim alikuwa Mkuu wa Skuli ya Kilimo, Kizimbani SUZA.

“Uteuzi huo unaanza leo tarehe 16 Novemba 2022,” imesema taarifa ya Mhandisi Zena.

error: Content is protected !!