December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge ajiuzulu kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Mbunge wa Rwanda, Gamariel Mbonimana

Spread the love

 

MBUNGE wa Rwanda, Gamariel Mbonimana ambaye alijiuzulu ubunge juzi tarehe 14 Novemba, 2022, ameomba msamaha kwa kuendesha gari akiwa mlevi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Jumatatu bunge la nchi hiyo liliidhinisha kujiuzulu kwake kwa sababu binafsi ikiwa ni siku moja baada ya Rais Paul Kagame kumkosoa mbunge huyo ambaye hakumtaja jina, kwa kuendesha gari akiwa mlevi.

Aidha, katika taarifa aliyoiweka kwenye mtandao wa Twitter, Gamariel Mbonimana aliomba msamaha kwa Wanyarwanda na rais na kuongeza kwamba ameamua kuacha pombe.

Mbonimana hakueleza zaidi kuhusu msamaha wake lakini alithibitisha Shirika la Habari Uingereza BBC kwamba ujumbe huo wa Twitter ni wa kwake.

Uendeshaji gari ukiwa mlevi una adhabu ya faini ya faranga 150,000 za Rwanda sawa na dola za Marekani 140 lakini adhabu ya kwenda jela kwa muda wa siku tano chini ya ulinzi wa polisi imeongezwa kwa wale wanaokamatwa makosa hayo.

Mwishoni mwa wiki, Kagame alikosoa polisi kwa kutomkamata mbunge huyo kwa sababu ya kinga yake.

Mbonimana alikuwa mbunge tangu 2018. Ni mwanachama wa Liberal Party – chama mshirika wa chama tawala cha Kagame (RPF).

Makamu wa rais wa chama chake Théogène Munyangeyo ameambia shirika la utangazaji la serikali ya Rwanda kuwa hawajawahi kumuona akinywa pombe hapo awali.

error: Content is protected !!