Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Waandishi wa habari wapewa wito kuondosha dhana potofu chanjo Uviko-19
Afya

Waandishi wa habari wapewa wito kuondosha dhana potofu chanjo Uviko-19

Spread the love

 

WAANDISHI wa Habari nchini Tanzania wamepewa wito wa kuishawishi jamii na kuondosha dhana potofu juu ya chanjo ya Ugonjwa wa uviko -19. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne Tarehe 18 Oktoba 2022 na  Ofisa Afya wa Mkoa wa Dar es Salaam Enezael Ayo, alipolipokuwa anawasilisha mada kwenye semina ya siku moja kwa waandishi wa habari jijini hapa iliyoratibiwa na Shirika la Internews na Klabu ya Waandishi wa habari Dar es Salaam (DCPC).

Enezael amesema kuwa baadhi ya viongozi wa dini waliwahi kutoa taarifa zilizopotosha umma juu ya chanjo hiyo ilhali chanjo hiyo ni salama.

“Waandishi wa Habari mtusaidie kuondosha dhana potofu juu chanjo kwa sababu hakuna mtu yoyote aliyepata madhara tangu chanjo hizi zilivyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Enezael.

Ametaja changamoto nyingine ni ya watu kujisahau baada ya kuona kiwango cha maambukizi kimeshuka na kwamba wengi wameacha utaratibu wa kuchukua tahadhari za kunawa mikono , kujisafisha kwa kitakasa mikono na kuvaa barakoa.

Amesema kuwa tangu Tanzania kuingia kwenye hatua za kuchukua tahadhari za ugonjwa huo maradhi mengi yalipungua kama vile kipindupindu.

Amezitaja takwimu za watu waliochanja jijini Dar es Salaam ambapo tayari wameshachanjwa ni zaidi ya watu Milioni mbili sawa na asimilia  85 huku malengo yakiwa ni watu 3,331,079.

Amesema kuwa wataalam wa Afya walishirikiana na watoa huduma ngazi ya jamii, wenyekiti wa serikali za mitaa kwa kufanya kazi ya kuhamasisha chanjo nyumba kwa nyumba pamoja na hamasa ya waandishi wa habari.

Naye Dk. Christina Mdingi mtaalam wa masuala ya afya ametoa msisitizo kwa waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele ili kuhakikisha kuwa wananchi wanabaki salama.

“Tuwajengee  wananchi tabia ya kuamini na kutekeleza yale yanayohadharishwa na wataalam wetu wa afya”

“Wanahabari wakikosea sentensi moja tu jamii imekwisha, jamii inawaamini sana kwa hiyo nyie watu muhimu kwenye hili,” amesema Dk. Mdingi.

Nevile Meena mhariri na mwandishi wa habari mkongwe amewaeleza waandishi wa habari namna bora ya kuzikabili taarifa za upotoshaji.

Amesema kuwa changamoto kuwa kuhusu habari za chanjo ni uvumi, tetesi, na dhana potofu.

Amezitaja baadhi ya dhana zilizoenea ni pamoja na kuhusishwa chanjo na ugonjwa huo na biashara, watu waliochanjwa kugeuka mazombi, na chanjo zenye majina tofauti.

Meena amesema kuwa kuliibuka taarifa nyingi za upotoshaji juu ya chanjo ya Uviko 19 siku chanjo hizo zilipofika nchini.

“Kazi ya serikali inafanana na ile ya mzazi ya kuhakikisha watoto wake wapo salama  hivyo Rais hawezi kukubali wananchi wake wafe,” amesema Meena.

Amesema kuwa waandishi wa habari wakifanya kazi zao vizuri wataondosha dhana potofu iliyojengwa kwa umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Kambi ya matibabu ya kibingwa Ruangwa yaacha vilio, DC atoa ombi JAI

Spread the loveMKUU wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma amefunga rasmi kambi...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Afya

Mbunge ataka huduma Ultrasound itolewe bure kwa wajawazito

Spread the loveMBUNGE wa Viti Maalum, Esther Malleko, ameitaka Serikali kutoa bure...

Afya

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!