Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wasafiri Tanzania kwenda Hong Kong hawatalazimika kukaa karantini
Habari za Siasa

Wasafiri Tanzania kwenda Hong Kong hawatalazimika kukaa karantini

Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam
Spread the love


MAMLAKA ya Hong Kong, imewaondolea sharti la kukaa karantini wasafiri kutoka nchini Tanzania wanaofanya safari zao mbalimbali nchini humo. Anaripoti Felister Mwaipeta TUDARCo … (endelea)

Hatua hiyo imethibitishwa na Balozi wa Tanzania , China  Mbwelwa Kairuki,  kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter leo Septemba 27.

Amesema wasafiri wote wanaofanya safari mbalimbali za kijamii na kiuchumi kutoka nchini Tanzania kuelekea Hongkong, China kwasasa hawatakiwi kufanya utaratibu wa kuishi karantini kama ilivyokuwa hapo awali kutokana na uwepo wa maambukizi ya virusi vya UVIKO-19 yaliyo sambaa duniani kote kuanzia mwaka 2020.

Katika andiko lake balozi Kairuki amesema hapo awali wasafiri wote waliokuwa wakifanya safari zao kuelekea Hongkong, na China walitatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka husika ya nchi hiyo ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona kwa kuishi karantini na kutochangamana na raia wengine.

Amesema hatua hiyo iliyofanywa na Mamlaka itawasaidia wafanyabiashara mbalimbali kufanya safari zao kiurahisi na kupata bidhaa zitakazokuza uchumi wao na nchi kwa ujumla hivyo, “watanzania wasihofie kufanya safari zao kuja Hongkong kwasasa.”

Aidha amesema uamuzi uliofanywa na Mamlaka ya Hongkong, kufuta sharti la kukaa karantini kwa wanao safiri kutoka Tanzania,  kuelekea nchi hiyo, “kutapunguza gharama za usafiri kuelekea bara, China kupitia  Hongkong, ” amesema Kairuki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!