Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgodi mkubwa wa dhahabu kuanzishwa Sengerema
Habari Mchanganyiko

Mgodi mkubwa wa dhahabu kuanzishwa Sengerema

Mgodi wa Buzwagi
Spread the love


MKUU wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima, amesema Serikali imeingia kwenye makubaliano na kampuni ya OA Coal ambayo itajenga mgodi wa pili kwa ukubwa baada ya Geita ambao utakuwa wilaya ya Sengerema. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo … (endelea).

Hayo ameyasema leo Jumatatu ya tarehe 26 Septemba 2022 katika mkutano wa kujadili na kuzitambua fursa zilizopo Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza fursa zilizopo katika mkoa huo Malima amesema, wananchi wanatakiwa watambue fursa zilizopo, kuzipokea na kuzichangamkia ili kusaidia ukuaji wa mapato ya uchumi kwa mkoa wa Mwanza na kuwafaidisha wananchi wengine wote.

Akizungumzia sekta ya uvuvi Malima amesema wananchi wametumia vibaya Ziwa Victoria kwani miaka 50 iliopita Ziwa hilo lilikuwa na aina takribani 40 ya Samaki lakini kwa sasa zimebaki aina 5 mpaka 6 ya samaki kutokana na uvuvi haramu. 

Pia amesema serikali ya mkoa wa Mwanza imejipanga kuongeza tija katika ufugaji ili waweze kukuza uzalishaji wa maziwa ambayo ni changamoto kubwa kwa wafugaji wengi.

Aidha, amesema pamoja na kuonesha fursa hizo kwa wakazi wa Mwanza jukumu lililopo ni kuwatoa wananchi gizani kwa kufanya utafiti wa masoko na kuwahakikishia uwepo wa masoko ili waongeze jitihada katika utendaji wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!