Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya HKMU, WKU kushirikiana kwenye tafiti za kitaaluma
Afya

HKMU, WKU kushirikiana kwenye tafiti za kitaaluma

Spread the love

 

CHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Western Kentucky cha Marekani (WKU) kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano katika taaluma baina ya vyuo hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yalisemwa jana chuoni hapo jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Yohana Mashalla, wakati ujumbe wa chuo hicho ulipotembelea HKMU Mikocheni Dar es Salaam.

Prof. Mashalla alisema kwenye ushirikiano huo watajikita kwenye tafiti mbalimbali za masuala ya afya na kuandika mapendekezo ya kuomba fedha kuwezesha kufanya tafiti zinazohitajika nchini.

Alisema ushirikiano huo utaijengea uwezo mkubwa HKMU wa kuandika maandiko ambayo yanaweza kuwavutia wadau mbalimbali duniani kutoa fedha za kusaidia tafiti kwenye masuala mbalimbali.

“Sisi HKMU tuna malengo matatu, kufundisha, kufanya tafiti na kutoa ushauri kwenye taasisi za serikali na mashirika ya nje kwa kutoa mawazo na uzoefu wetu kwenye nyanja mbalimbali hivyo ushirikiano huu utatujengea uwezo kutoa ushauri mzuri kwa serikali na wengine,” alisema Prof. Mashalla.

Alisema kwenye mazungumzo yao wamebadilishana uzoefu wa namna ya kufundisha na teknolojia za aina mbalimbali zinazotumika kufundishia wanafunzi wa udaktari, uuguzi na fani zinginezo.

“Uhusiano huu unamanufaa kwetu na kwao kwa sababu kwa dunia ya sasa ni ngumu sana taasisi kuishi kama iko kwenye kisiwa hivyo lazima taasisi zishirikiane. Hapa tunasikilizana wao wana kozi gani nasisi tunakozi gani tushirikiane kuanzisha program ambazo wao wanazo sisi hatuna,” alisema

Alisema kupitia ushirikiano huo watakuwa na utaratibu wa kubadilishana wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho kwa wao kuja kufundisha kwa muda kwenye fani ambazo hazina wataalamu wengi nchini.

Profesa William Mkanta, ambaye ni mtanzania anayefanyakazi kwenye chuo hicho cha WKU, alisema aliamua kuwaunganisha ili waweze kushirikiana kwenye tafiti zenye manufaa kwa jamii.

“Mimi ni mzaliwa wa Tanzania ila nafanya kazi Marekani kama Profesa, nimeona umuhimu wa vyuo vikuu kusaidia jamii kwasababu vyuo vikuu ndiyo kitovu cha utafiti, huduma na kitovu cha kujifunza.

“Ndiyo maana tumeona tuwe na uhisino wa vyuo hivi ili tuweze kuhamisha vipaji vilivyopo kwenye vyuo hivi. Dunia ni kama kijiji siyo lazima watu majirani ndiyo mshirikiane bali hata walio mbali wanaweza kushirikiana ndiyo maana tumeona umbali uliopo baina ya HKMU na WKU siyo kikwazo cha ushirikiano,” alisema Prof. Mkanta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mbunge ataka huduma Ultrasound itolewe bure kwa wajawazito

Spread the loveMBUNGE wa Viti Maalum, Esther Malleko, ameitaka Serikali kutoa bure...

Afya

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

AfyaHabari za Siasa

Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Afya, imeliomba Bunge lipitishe makadirio yake ya mapato...

AfyaHabari za Siasa

Vifo vitokanavyo na UKIMWI vyapungua

Spread the loveVIFO vinavyosababishwa na Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), vimepungua kutoka...

error: Content is protected !!