October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shaka: Muungano ni ngao ya Taifa

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesema chama chochote cha cha siasa chenye shauku ya kuvunja Muungano au viongozi wake wakipania kuligawa Taifa huo si ushujaa bali ni kuishiwa hoja, upeo mdogo na maarifa duni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Katibu wa NEC itikadi na Uenezi shaka Hamdu Shaka jana aliwaeleza waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao cha kamati Maalum ya NEC kilichoketi mjini Unguja alipotakiwa kutoa mtazamo wake juu ya kauli ya baadhi ya wanasiasa hivi karibuni kudai ili zanzibar iweze kutawala ni vyema kuwa na mamlaka kamili ya kimaamuzi..

Shaka alisema wapo baadhi ya viongozi wa upinzani kwa muda mrefu wako katika juhudi za kushawishi wananchi waone Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna maana na wala si muhimu jambo ambalo ni upotishaji mkubwa.

Amefahamisha kuwa aina ya wanasiasa hao hawana hoja za msingi kuwaeleza wananchi badala yake wamekuwa na kazi ya kuwajaza chuki na matumai hewa ambayo hawana ubavu nayo wala uwezo wa kubadili lolote .

“Katika uongozi na siasa viongozi mkishindwa kufikia matlaba yenu jamii huwapuuza .Wapo watu bila muungano wasingepewa hata usheha . Kutambulika kwao na sauti zao kusikika kwao ni kuwepo kwa muungano ambao leo wanaudhihaki na kuona sio lolote wala chochote kutokana na ubinafsi wao wa nafsi “Alisema shaka

Katibu huyo Mwenezi alisema hata ustawi wa utulivu, amani na umoja katika pande mbili za Muungano kunatokana na uimara wa muungano kwani nje ya muungano si Tanganyika wala Zanzibar zitakazobaki salama.

“Ndani ya Muungano kuna uhuru wa kutosha na watu wakiishi kwa amani. Nje ya Muungano usalama utapeperuka. Utulivu wa ndani na wa kisiasa utakosekana. Tusikubali kukichoma kichaka cha Muungano tutakosa mahali pa kujihifadhi ” Alisisitiza Shaka

Aidha amefafanua kuwa hata baadhi ya mataifa ya ulaya Mashariki yalipokuwa chini ya umoja wa kisoviet yaliojiona yako jela na USSR ilipogawanyika yakajikuta yakigeuka na baadhi yao sasa wamekuwa wakala wa ushetani.

“Tuna baadhi ya wanasiasa wetu wako tayari hata kuuza utu wao ili wamtumikie shetani aliye kizani. Watu hao kwa bahati nzuri ni wachache wenye uchu wa madaraka. Wangeungwa mkono na wengi tungalizamishwa au kupigwa bei mnadani “Alielezea

Mwenezi huyo wa CCM aliongeza kusema huku aliwatahadharisha wananchi wa unguja na pemba kuendelea kuwa makini kwa kile alichokiita kutahadhari macho yao ili kulinda umoja ulipo usipeperushwe na kimbunga Katrina .

Hata hivyo Shaka amesifu uongozi bora, makini na wenye uthubutu wa kusimamia sera za mageuzi ya kiuchumi Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Mwinyi .

Amewataja viongozi hao kuwa wametawaliwa na Uvumilivu, uchapakazi na wanatekeleza wajibu wao kwa kufuata malengo ya kisera yaliowekwa na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya 2020-2025 jambo ambalo limeendelea kuwafanya wananchi kuwa na imani kubwa na serikali na Cha Cha Mapinduzi.

error: Content is protected !!