KUFUATIA mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchi jirani ya Uganda, Serikali ya Tanzania imewaondoa hofu wananchi wake kwa kueleza kuwa hakuna kisa hata kimoja na imeanza kuchukua hatua za tahadhari. Anaripoti Jonas Mushi…(endelea)
Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola jana tarehe 20 Septemba, 2022, baada ya watu kadhaa kuripotiwa kufariki kwa ugonjwa huo unaosababishwa na kirusi cha Ebola.
Katika taarifa yake kwa umma leo Jumatano tarehe 21, 2022, Naibu Waziri wa Afya wa Tanzania,, Godwin Mollel amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini humo lakini akawataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Amesema kuwa tayari amewaagiza waganga wakuu wa mikoa na halamashauri nchini humo kuimarisha utoaji eleimu, ufuatiliaji wa ugonjwa huo, uchunguzi w akitaalamu na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba na kinga muhimu katika maeneo yao.
“Vilevile nimeagiza kuimarisha uchunguzi wa wageni wanaoingia nchini kupitia mipaka yetu ikiwemo matumizi ya vipima joto,” amesema Mollel.
Leave a comment