Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia, Nyusi wakubaliana kuongeza ushirikiano usalama, ulinzi
Habari Mchanganyiko

Rais Samia, Nyusi wakubaliana kuongeza ushirikiano usalama, ulinzi

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Msumbiji, Filipe Nyusi wamekubaliana kushirikiana katika eneo la ulinzi na usalama ili kuondokana na changamoto ya ugaidi, biashara haramu ya binadamu na dawa za kulevya. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumatano tarehe 21, 2022 na kutiliwa saini Ikulu ya Maputo nchini Msumbiji ambapo Rais Samia yupo kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Rais Samia alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbji katika masuala ya usalama na ulinzi ulianza tangu mwaka 1980 na kwamba ni muhimu kuuimarisha.

“Kupitia mahusiano haya tumewweza kutiliana saini eneo la usalama na ulinzi na utafutaji na uokoaji na ni hatua muhimu katika kusonga mbele,” amesema Rais Samia.

Amesema kumekuwepo na uhalifu mkubwa wa mipakani ikiwemo suala la ugaidi ambao unaendelea na kwamba kutokana na urefu wa mpaka huo kuna umuhimu mkubwa wa kushirikiana.

Kwa upande wake, Nyusi katika hotuba yake kwa waandishi wa habari amesema sheria na mikataba ya ushirikiano inahitajika katika kukabiliana na ugaidi.

Amesema makubaliano yao yanagusa maeneo mengi ikiwemo dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu na mambo yanayoendana na hayo.

Aidha, amesema katika eneo la biashara kumekuwa na kuzorota nchini Msumbiji ambayo inapitia wakati mgumuikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mbali na usalama na ulinzi nchi hizo pia zimekubaliana kushirikiana katika masuala ya elimu ikiwemo ufundishaji wa lugha ya Kiswahili.

Pia wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara ambapo imeelezwa kushuka kutoka Sh 53 bilioni hadi Sh 36 bilioni mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

error: Content is protected !!