Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Mpango ataka udhibiti dawa za kuhifadhi samaki
Afya

Dk. Mpango ataka udhibiti dawa za kuhifadhi samaki

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amezitaka mamlaka za udhibiti kukomesha matumizi ya dawa zisizofaa katika uhifadhi wa samaki ili kuepukana na ongezeko la wagonjwa wa saratani katika mkoa wa Mwanza. Anaripoti Erick Mbawala, TUDARCo … (endelea).

Dk. Mpango ameyasema hayo leo tarehe 13 Septemba, 2022 akizindua jengo la wodi ya wagonjwa wa saratani, katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Bugando, Jijini Mwanza.

Ametoa msisitizo huo pia kwa wakazi wa mkoa huo ambao wanajishughulisha na Uvuvi.

Amesema serikali inawekeza katika ujenzi wa miundombinu ili kuhakikisha huduma za saratani zinasogezwa karibu na wananchi.

Ameongeza kwamba takwimu zinaonesha kuwa ugonjwa wa saratani bado ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza duniani kwa kusababisha vifo vya watu wengi.

Amesema Tanzania ina takribani watu 42,000 kila mwaka hupata ugonjwa wa saratani.

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango

Mpango pia amelishukuru kanisa katoliki na madhehebu mengine kwa kuendelea kushirikiana na serikali kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi hususani huduma za afya na kuongezea kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wengine ili kuendelea kuboresha huduma za afya.

Tanzania imekuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa afrika Mashariki kuanzisha kiwanda cha Mionzi Dawa kitakachosaidia utoaji huduma kwa wagonjwa wa Saratani ndani na nje ya nchi.

Aidha, Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Fabian Masanga amesema kukamilika kwa jengo hilo kutaleta unafuu kwa wananchi wa kanda ya ziwa, kupungua kwa gharama za wagonjwa waliokuwa wakipata malazi nje ya hospitali, pamoja na wagonjwa kufuatilia huduma za matibabu kwa urahisi zaidi.

Naye Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bugando, Mhashamu Renatus Nkwande ameishukuru Serikali kwa kushirikiana na Kanisa hilo katika kuhudumia wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya.

Pia ameiomba Serikali iendelee kuisaidia hospitali hiyo kupata mashine na vifaa mbalimbali ili kuboresha utoaji wa huduma za matibabu ya ugonjwa wa saratani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mbunge ataka huduma Ultrasound itolewe bure kwa wajawazito

Spread the loveMBUNGE wa Viti Maalum, Esther Malleko, ameitaka Serikali kutoa bure...

Afya

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

AfyaHabari za Siasa

Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Afya, imeliomba Bunge lipitishe makadirio yake ya mapato...

AfyaHabari za Siasa

Vifo vitokanavyo na UKIMWI vyapungua

Spread the loveVIFO vinavyosababishwa na Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), vimepungua kutoka...

error: Content is protected !!