Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lipumba ateua viongozi wapya CUF
Habari za Siasa

Lipumba ateua viongozi wapya CUF

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba  amemteua Rashid Sudi Khamis, kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama hicho huku Nawiya Abdallah Mussa, akiteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2022 na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, uteuzi wa wakurugenzi hao utakamilika baada ya wahusika kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho.

“Mwenyekiti wa CUF, Prof. Lipumba baada ya kushauriana na makamu wake na kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 94 ya Katiba ya CUF, toleo la 2019, amefanya uteuzi wa wakurugenzi wawili,” imesema taarifa ya Mhandisi Ngulangwa.

Taarifa ya Mhandisi Ngulangwa imesema, Khamis ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anaishika, Mbarouk Seif Salum, kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar.

Naye Nawiya amteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, kushika nafasi ya Khadija Makontena aliyefarikia dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!