Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kundi la tano kaya 25 kutoka Ngorongoro mbioni kuhamia Msomera
Habari Mchanganyiko

Kundi la tano kaya 25 kutoka Ngorongoro mbioni kuhamia Msomera

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu nchini Tanzania, Balozi Pindi Chana
Spread the love

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana amesema kundi la tano la wakazi wa Ngorongoro takribani kaya zisizopungua 25 kwa sasa lipo kwenye mchakato wa kuhama kwenda Msomera mkoani Tanga kwa hiari. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo … (endelea).

Amesema hayo leo Ijumaa ya tarehe 19 Agosti 2022, katika hafla ya kuhamisha wananchi wa Ngorongoro awamu ya pili Kwenda Msomera kwa hiari kwa lengo la kuiacha Ngorongoro ibaki kama eneo la hifadhi kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Amebainisha kuwa shughuli za uhifadhi zinachangia takribani asilimia 17 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato ya nje, ambapo inasaidia kuleta maendeleo kama ujenzi wa miundombinu ikiwemo elimu na afya.

Amesema kuwa kitendo cha wananchi hao kukubali kwa hiari kuhama kitawanufaisha kwani kwa kuzingatia haki za wananchi hao watajipatia haki zao za msingi ikiwemo umiliki wa ardhi ambapo katika eneo la hifadhi wananchi hawaruhusiwi kumiliki ardhi.

Pia ameeleza kuwa wananchi watajipatia maendeleo ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule, vyuo vikuu na VETA.

Amethibitisha kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri kwani upo utaratibu mzuri wa kusafirisha watu na mifugo. Pia miundombinu pamoja na nyumba zipo tayari katika eneo la Msomera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!